WANAHABARI HUBIRINI HAKI ZA BINADAMU

  WANAHABARI HUBIRINI HAKI ZA BINADAMU Waandishi wa habari wametakiwa kufichua vitendo vya ukiakaji wa haki za binadamu na kuwatetea wanyonge kwa kupaza sauti kwenye vyombo vyao vya habari wanavyovinyia kazi. wito huo umetolewa na mkurugenzi mtendaji wa Mtandao wa Ulinzi wa Watetezi wa Haki za Binadamu(THRD), Onesmo Olengurumwa, ambapo alisema waandishi wa habari wanapaswa kuwa mstari wa mbele kufichua vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu Mkurugenzi huyo aliyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya siku tatu kwa waandishi wa habari wa mikoa ya Lindi,Mtwara na Ruvuma yanayofanyika katika ukumbi wa VETA mjini Mtwara. Olengurumwa alisema kundi kubwa la wananchi wanyonge halina eneo linalotegemea sauti yake kupazwa na kusikika,zaidi ya waandishi habari kupitia vyombo vya habari. Alisema  serikali inavyombo vyake vya kuisemea na kuitetea lakini wananchi ambao wengi wao ni wanyonge,hivyo kalamu za waandishi ni tumaini lao katika kuwatetea. Aidha Olengurumwa aliwakumbusha waandishi hao kuandika habari bila upendeleo na kwakuzingatia uandishi wa amani badala ya uchochezi.” katika kuandika  nivizuri mchukue tahadhari na kuweni waangali fu,tendeni haki  pateni taarifa za kila eneo kuhusiana na habari husika bila kuegemea upande mmoja,” alisema Olengurumwa. Mkurugenzi huyo aliongoza  kusema uandishi wa amani na unaozingatia haki utawafanya waaminiwe na jamii na hata vyombo vyenye mamlaka kiutawala ili kuepuka kuitwa wachochezi na majina mengine yasiyofaa,hasa wakati wa kupiga kura za maoni kwa katiba inayopendekezwa na uchaguzi mkuu ujao.” mwaka huu unahekaheka nyinyi  ambazo  siyo salama sana kwa waandishi na watetezi wa haki za binadamu,kuweni waangalifu kwani kuna suala la kura za maoni na uchaguzi mkuu,” alionywa Olengurumwa.Mafunzo hayo  ya siku tatu kwa baadhi ya waandishi wa habari  mikoa ya Lindi,Mtwara na Ruvuma yameanza leo katika mji wa manispaa ya Mtwara yanatarajiwa kumalizika tarehe 6 mwezi huu. MWISHO.

Rate this:

Permalink

MARUFUKU KUKATA PESA ZA WAKULIM SERIKALI mkoani Mtwara imepiga marufuku kwa vyama vya msingi na mabaraza ya madiwani mkoani hapa kuweka utaratibu wa kukata pesa kutoka katika malipo ya tatu ya mauzo ya… Continue reading

Rate this:

WANAKIKUNDI WA TANGAZO KUJENGEANA NYUMBA

WANACHAMA wa kikundi cha Jitegemee kilichopo katika kijiji cha Tangazo wilayani Mtwara mkoani hapa, wameazimia kujengeana nyumba bora za kisasa ili kuboresha maisha yao na kuendena na mabadiliko yanayotokea kwa sasa.   Akiongea… Continue reading

Rate this:

Masasi, Nanyumbu wapongezwa ujenzi wa maabara

SERIKALI mkoan Mtwara imeridhishwa na kasi ya utekelezaji wa agizo la Raisi kikwete juu ya ujenzi wa maabara katika shule za sekondari za kata, hasa katika wilaya za Masasi, Nanyumbu na masasi mjini.… Continue reading

Rate this:

VIJANA MTWARA WACHANGAMKIA FURSA

ZOEZI la uchukuaji fomu kwaajili ya vijana mbalimbali kushiriki katika Shindano la Mashujaa wa Kesho la Statoil limeendelea kushika kasi huku idadi kubwa ya vijana wakiendelea kurejesha fomu kwa lengo la kushiriki katika kinyang’anyiro hicho.   Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, AfisaMawasilianowa Statoil Tanzania, Erick Mchome alisema hadi sasa zaidi yavijana 150 tayari wamerejesha fomu zao tayari kwa kuyashindanisha mawazo anuai ya miradi yao walio iwasilisha kwaajili ya kushiriki katika shindano hilo.   Mchome alisema vijana hao wamejaza fomu kwaajili ya kushiriki katika shindano hilo kuwania kitita cha Dola 5,000 kwa mshindi wa kwanza”.   “Kimsingizoezihili la shindano la Mashujaa wa… Continue reading

Rate this:

CHANGAMKIENI FURSA

VIJANA Mkoani hapa wametakiwa luchangamkia fursa ya ujasiriamali inayoletwa na Shirika la utafutaji wa gesi la Statoil kwa kuandika wazo la biashara na kushindanishwa ili kupata moja litakaloweza kupatiwa mtaji. Wito huo umetolewa… Continue reading

Rate this:

SHIKAMANENI KATIKA UMOJA

SHIKAMANANI KATIKA UMOJA   WANACCM wilayani kupitia jumuiya zote za chama hicho Newala mkoa wa Mtwara wameshauriwa kuwa na umoja na  kushirikiana na kuwa na upendo miongoni mwao ili kuhakikisha wanapata ushindi wa… Continue reading

Rate this:

Permalink

WATOTO WANAOTUMIKISHWA   JAMII ya wakazi wa mkoa wa Mtwara wenye uwezo kiuchumi wameaswa kujenga tabia ya kujitolea kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi ili kuwawezesha kuishi maisha mazuri hapo baadae badala ya… Continue reading

Rate this:

NANYAMBA NA UTAWALABORA

NANYAMBA NA UTAWALA BORA KUTOKUWAPO kwa uadilifu miongoni mwa watendaji wa vijji,uelewa mdogo wa wananchi juu ya masuala ya utawala na wanasiasa kutoshiriki katika kuhamasisha jamii kuhudhuria katika mikutano ya vijiji ni miongoni… Continue reading

Rate this:

WATIMUENI KWA ADABU VIONGOZI WENU

MSIWATIMUE HOVYO VIONGOZI WENU WAKAZI wa vijiji vya kata na tarafa ya Nanyamba wilaya ya Mtwara mkoani hapa, wameaswa kutowatimua madarakani viongozi wao wa vijiji na vitongoji au kuwazomea mbele ya viongozi wa… Continue reading

Rate this: