MURJI AJIPANGA UCHAGUZI CCM
Chaguzi zitukomboe kwenye umasikini, Mhe; unaona hali hii

MBUNGE wa Mtwara mjini Asnain Murji amewataka wanachama wa CCM kumaliza tofauti zao zilitokana na majeraha ya uchaguzi uliopita na kwa sasa waangazie katika kuwapata viongozi bora ndani ya chama hivyo kikongwe barani Afrika


Murji ameweka wazi msimamo wake wa maandalizi ya uchaguzi huo unaotarajia kufanyika mwakani (2012) leo wakati akiwasilisha taarifa yake ya utekelezaji wa ahadi binafsi alizozitoa wakati wa kampeni za uchaguzi uliomweka madarakani.


Murji licha ya kujigamba kuwa katika kipindi cha miezi kumi ya uongozi wake amefanya mambo makubwa kwa wananchi likiwemo kutoa magari mawili kwa ajili ya kusafirisha wanafunzi bure, alisema ni vibaya kuendeleza chuki za uchaguzi uliopita.


“uchaguzi umekwisha sasa tuijenge Mtwara yetu, nafahamu tulitofautiana sana, ila sasa tukubali kuwa mbunge ni mimi…tuangalie uchaguzi wa chama, wakati tunaelekea huko yatupasa kujiuliza nguvu ya upinzani (CUF) kwenda mahakamani waliipata wapi kama sio kutoka miongoni mwetu” alisema Murji


“Wanachama wenzangu tuwekeze nguvu zetu katika kuwapata viongozi bora watakaokiondoa chama chetu katika wakati mgumu…CCM ni miongoni mwa vyama vichache barani Afrika ambavyo ni vikongwe, sasa lazima tuwe makini vinginevyo itatufia” alisisitiza


Mwisho