WALIOIBA MITIHANI NAO WAMEFELI

WANAFUNZI 22 kati ya 413 waliofutiwa matokeo ya mitihani ya darasa la saba mwaka huu mkoani Mtwara wamefeli licha ya kubainika kuwa

Wanafunzi wa shule ya Msingi Mangaka mkoani Mtwara wakitafuta elimu bora

walitazamia majibu ya mitihani hiyo.

Hayo ayamebainishwa leo (jana) na ofisa elimu wa mkoa wa Mtwara, Hipson Kipenya wakati alipokuwa akitangaza matokeo ya mitihani ya darasa la saba mwaka huu, hafla iliyofanyika shule ya sekondari ya wasichana Masasi.

Kipenya alisema kuwa halmashauri tano kati ya sita za mkoa wa Mtwara zimebainishwa na baraza la mitihani kuwa zilijihusisha na udanganyifu  wakati wa kufanya mitihani hiyo Septemba, mwaka huu.

“Wanafunzi 22 kati ya 413 waliofutiwa matokeo ya mitihani yao walifeli…yaani licha ya kuangalizia majibu bado wameshindwa kufaulu…ni wilaya ya nanyumbu tu ambayo haijahusika na vitendo hivyo, idadi hiyo ni kati ya wanafunzi 9000 waliofutiwa matokeo kitaifa” alisema Kipenya na kuongeza

Alizitaja shule hizo na wilaya zake katika mabano kuwa ni Mangamba (Mtwara Manispaa), Libobe, Mnyija (Mtwara), Amani, Mihambwe, Mwangaza (Tandahimba), Mnauya (Newala) na Huwe,Kambarage, Masasi, Nangoo na Ng’uni (Masasi)

“Kamati ya mitihani ya mkoa imewaagiza Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri husika kuwavua madaraka ya ukuu wa shule walimu wakuu husika, pamoja na kuwapa onyo kali wasimamizi wa mitihani hiyo…hizi ni hatua za awali” alisisitiza ofisa elimu huyo

Ofisa Elimu wa mkoa wa Mtwara Hipson Kipenya akiwasilisha mada juu ya hali ya elimu mkoani humo hivi karibuni

Hata hivyo alisema mkoa umefanikiwa kuongeza kiwango cha ufaulu kutoka asilimia 47. 7 mwaka jana na kufikia asilimia 50.2 baada ya wanafunzi 15,947 wakiwemo wavulana 8,078 na wasichana 7869 kufaulu kati ya 31,795 waliofanya mitihani hiyo.

Alisema mwaka 2005 jumla ya wanafunzi 40,310 wakiwemo wavulana 15,588 na wasichana 17,621 sawa na asilimia 82.4 waliandikishwa kujiunga na darasa la kwanza ambapo kati yao 7,101 sawa na asilimia 17.6 hawakuweza kufanya mitihani hiyo.

“Mkoa una nafasi 16,836 za wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2012 katika shule za sekondari za kutwa na bweni, nafasi hizi ni swan a asilimia 52.9 ya wanafunzi 31,795 ya wanafunzi waliofanya mtihani, kutokana na hali hiyo mkoa una nafasi wazi 889” alibainisha Kipenya.

Alifafanua kuwa “Manispaa ya Mtwara Mikindani inaongoza kwa kufaulisha asilimia 63.7, Mtwara 60.9, Tandahimba 59.6 Newala 44.0, Masasi 45.5 na Nanyumbu asilimia 37.7”

Kwa upande wake ofisa elimu mkuu, Sylvia Chinguile alionesha kukerwa na taarifa ya kubainika kwa uwapo wa udanganyifu katika mitihani hiyo na kuonya kuwa vitendo hivyo vitaliangamiza taifa.

“Haya mambo tulizoea kuyasikia mikoa ya kasikazini, leo yamehamia Mtwara, hebu jiulizeni iwapo wanafunzi wote 413 wangechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza hali ingekuwaje?…tusiliangamize taifa kwa kutengeneza wasomi wasio na uwezo” alionya Chinguile

Kikao hicho kilichoketi chini ya uwenyekiti wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara, Yusuf Matumbo kiliridhia matokeo hayo na kuzitaka wadau wa elimu mkoani hapa kuendelea kupambana na changamoto zinazorudisha nyuma sekta ya elimu.

Mwisho

Advertisements