MASASI WAKATAA UCHIMBAJI WA VISIMA

MWENYEKITI wa halmashauri ya wilaya ya Masasi, mkoani Mtwara, Jafari

Madiwani wa halmashauri ya Masasi, mkoani Mtwara-tupo makini

Mkwanda amesema hayupo tayari kuendelea kutekeleza miradi ambayo mikataba yake husainiwa mithili ya ukoloni ambayo Karl Peters na Chief Mangungu walisaini.

Mkwanda  ambaye ni diwani wa kata ya Chiwata alitoa msimamo huo kufuatia majibu yaliyotolewa na Mhandisi wa Maji wa wilaya hiyo, John Majura katika kikao cha baraza la madiwani kilichoketi mwishoni mwa wiki kuwa miradi ya maji inayofadhiliwa na wageni haiwezi kutekelezwa kinyume kwa kuwa mikataba imesainiwa kitaifa.

 “Kuna visima vinne tumepata maji, lakini kati ya hivyo kimoja tu ndicho kitajengewa mtandao wake, hivi vingine benki ya dunia wamesema vimekosa vigezo vya kupata fedha za ujenzi wa mtandao” alisema Majura

 Alifafanua kuwa “Ili kisima kijengewe miundombinu ya maji ni lazima kiwe na uwezo wa kutoa ‘cubic 6’ sawa na lita 6000 kwa saa, katika visima vyetu vinne ni kimoja tu cha Mkululu ndicho chenye sifa hiyo…hatuwezi kubadili msimamo huo kwa kuwa mikata inasainiwa kitaifa”

 Majibu hayo yalitokana na makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Juma Satima kuhoji sababu za miradi ya maji kuwa na fedha nyingi katika kitengo cha mtaalam mshauri huku fedha za utekelezaji wa mradi wenyewe zikiwa haba.

Mwenyekiti huyo alisema ni heri kuwa masikini jeuri kuliko kugeuzwa kuwa mkondo wa kunufaisha wachache na kwamba mikataba yote ambayo haitakuwa na maslahi ya umma hayupo tayari kuitekeleza.

“Heri kuwa masikini jeuri kuliko kuwa mkondo wa kunufaisha wachache, wanaleta fedha nyingi na wanazifuata kwa mgogo wa mtaalam mshauri, tumechoka na hali hiyo…sitaki mikataba ya Mangungu na Karl Peters” alisema mwenyekiti huyo

 Alisisitiza kuwa “Kuanzia sasa hatutaki miradi ya uchimbaji wa visima, nguvu zetu tunaelekeza katika uchimbaji wa mabwawa…visima vimetufikisha mahala ambapo tatizo la maji sugu”

Mwisho

Advertisements