SERIKALI YAHAHA KUZIMA HOJA YA UDINI NDANDA

 

ATIKA kile kinachoonekana ni jitihada za kuzika mgogoro wa udini

Naibu Waziri Elimu TAMISEMI Kassim Majaliwa akisisitiza jambo shuleni Ndanda

uliosababisha wanafunzi 20 kufukuzwa shule ya sekondari ya juu ya wavulana Ndanda, wilaya ya Masasi mkoani Mtwara serikali imetuma ujumbe wa kulipatia ufumbuzi tatizohilo.

Ujumbe huo uliwasili mjini Masasi jana ukioongozwa na Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) anayeshughulikia elimu, Kassim Majaliwa ulitumia zaidi ya saa kumi kuanzia saa 8 mchana hadi saa 5 usiku kujadili sualahilo.

Mbali na viongozi wa elimu ngani ya mkoa, ujumbe huo pia uliambata na Mwenyekiti wa Baraza Kuu la WaislamTanzania(Bakwata) mkoani Mtwara, Alhaji Marijani Dadi na katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma Idara ya Ualimu mkoani hapa, Samuel Zenda.

Wanafunzi wa Ndanda high school' wakimsikiliza Majaliwa

Akizungumza kwa nyakati tofauti katika vikao na viongozi wa serikali wa wilaya ya Masasi na baadye wanafunzi, Majaliwa alisema madai ya wanafunzi waislamu katika shule ya Ndanda yameishtua serikali hivyo ni lazima kuzika chembechembe za udini zinazojitokeza shuleni hapo.

“Sisi kama serikali tulishtushwa na taarifa kupitia vyombo vya habari kuwa wanafunzi wameandamana kutaka kujengewa mskiti shuleni, pia walikuwa wanatishia amani iwapo ombi lao halitatekelezwa” alisema Majaliwa

Aliongeza kuwa “Katika madaiyaoya pili wamesema hakuna usawa katika serikali ya wanafunzi shuleni hapo, wanataka usawa wa viongozi kwa kuzingatia dini zao na tatu wanadai mkuu wa shule ni mdini”

Mwenyekiti wa BAKWATA mkoa wa Mtwara Alhaji Marijani Dadi akisisitiza jambo shule ya sekondari Ndanda wilayani Masasi, Mkoani Mtwara

Alisema waokamaserikali hawana dini na kwamba si ujenzi wa Msikiti wala Kanisa utakaoruhusiwa katika eneo la shule za sekondari za serikali, licha ya kutambua umuhimu wa wananchi wake kuwa huru katika kuabudu.

“Tunaomba wanafunzi wetu waendelee na ibada zao katika vyumba vilivyotengwa na utawala…hili la serikali ya wanafunzi halina msingi wowote, ni vema wanafunzi watambue kuwa uongozi hautolewi kwa misingi ya dini bali uwezo wao…msilipe nafasi suala la udini mutatafutana hapa” alisema Majaliwa

Alisisitiza kuwa “Tumekubaliana na mkuu wa shule awabadilishie chumba cha ibada kwa sababu kilichopo ni kidogo…lililowaleta hapa kwanza ni elimu, lakinihilohaliondoi haki yenu ya kuabudu ndiyo maana serikali imeridhia kuwapo kwa mitihani ya dini”

Akiwa shuleni Ndanda kuanzia saa 11 jioni Naibu Waziri huyo alielezwa na Mwenyekiti wa Bodi ya ushauri ya shule hiyo, Agnes Mnenje kuwa katika kikao chake cha bodi Desemba, 21 mwaka jana kimewafukuza shule wanafunzi 20 katiyao16 wa shule ya wa kidato cha Sita na wanne wa kidato cha tano.

“Tuliwaandikia barua wanafunzi wote 21 waliobainika kuwa vinara wa mgogoro huo, ni wazazi na wanafunziTisatu ndiyo waliofika mbele ya bodi kuhojiwa ambapo wanafunzi wao walikubali kufanya kosa” alisema Mnenje

Mnenje alisema bodi hiyo ilipendekeza walimu waliohuska katika sulahilowahamishwe kitendo ambacho kimetekelezwa na halmashauri ya wilaya hiyo, ambapo mwalimu Salum Ummi amehamishiwa shule ya Namajani na Mtumwa Hassan alipelekwa Namombwe.

Katika hatua nyingine Bakwata limeiomba serikali kutumia busara kuwasamehe wanafunzi waliofukuzwa shule ili waweze kuendelea na masomoyao.

“Naomba serikali itumie busara wanafunzi hawa warejee shuleni, kamahilolinashindikana basi waruhusiwe kufanya mitihani, hawa ni watoto wetu na ndiyo taifa letu la kesho, sasa kuwafukuza shule sidhani kuwa tutakuwa tumewasaidia naombasanabusara zitumike” alisema Alhaji Marijani

Aidha katibu wa TSD, mkoani hapa Zenda alionesha kupingana na uwamuzi wa wilaya wa kuwahamisha walimu wawili wa shule hiyo ambao wanadaiwa kuchagiza wanafunzi katika madaiyao.

“Naomba mutambue kuwa serikali  ilipiga marufuku uhamisho wa adhabu, hawa wametenda kosa ninyi mumeona adhabu yake ni kuwahamisha…hilosi sahihi, waleteni kwenye mamlaka ya nidhamu na ikidhibitika atachukuliwa hatua sitahiki” alisema Zenda

Awali mkuu wa shule hiyo, Joseph Sowani  alisema wanafunzi hao Mbali na kufanya maandamano yaliyotia nanga ofisi ya mkuu wa wilaya, pia wanadiwa kutoa lugha ya vitisho kwa walimu hali iliyolazimu uongozi wa shule hiyo kuifunga kwa dharura Desemba, 5 mwaka huu ili kuruhusu uchunguzi kubaini chagizo la hali hiyo.

“Hali kwa sasa ni shwari tangu tufungue shule Desemba, 27 mwaka jana na zaidi ya wanafunzi 500 wameripoti shuleni na wanaendelea na masomo baada ya kujaza fomu za masharti na sheria za shule” alisema Sowani

Mwisho

Advertisements