UGUMU WA MAISHA HADI LINI?

Hali ya maisha imezidi kuwa ngumu kila uchao, bei ya vyakula imepanda kuliko mazao ya biashara, mfano mchele kwa sasa unauzwa kati ya sh. 200 hadi 2200 kwa soko kuu la Mtwara, bei hii ni ya juu zaidi ukilinganisha na bei za korosho ambalo ni zao kuu la biashara 1200 kwa kilo.

Shuhudia bei za mchele mjini Mtwara

Rais Jakaya Kikwete anawapa hi

Unga umefikia kati ya 1000 hadi 1200, bei hii inafanana na ile ya korosho, lakini sukari imepaa na kufikia kati ya 2500 hadi 3000 hizi ni bei za Mtwara, kimsingi hakuna sababu ya sukari kuuzwa kwa bei hiyo kwa sababu viwanda tunavyo, kile cha Mtibwa na kule Kirombelo bila kusahau Tanga.

Hali ya ugumu wa maisha inajitokeza wakati ambapo watawala wapo kimya huku badala ya kuchukua hatua wamekuwa wakilalamika, hivi ndiyo kusema watawala wameshindwa kazi?

Katika mada hii nataraji wewe msomaji tujadili kwa pamoja, nini mtazamo wako, nini kifanyike

Usomaji mwema

Advertisements