NANI KARUHUSU WATOA UCHAWI MTWARA KUKAMATWA?

Ni kitendawili kigumu kutengua ili kujua nani ameruhusu kukamatwa kwa waganga wa jadi wanaotoa uchawi katika manispaa ya Mtwara Mikindani.

Mambo ya utoaji uchawi. picha na maktaba yetuPicha inayosadikiwa ni za kichawi

picha inayoakisi matendo ya kichawi

Katika macho ya haraka haraka unaweza kusema ni RPC au OCD ndiye aliyeruhusu lakini kwa mtazamo mpana unaweza kujiuliza kuwa shughuli hizo hazikuanza leo wala jana mbonaka kama ni RPC au OCD hakukamata pale walipofanya shughuli hizo, kule Mikindani, Majengona maeneo mengine ya Mtwara mjini? ukiachilia mbali Naumbu nyumbani kwa Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Hawa Ghasia.

Swali la msingi la kuhoj ni kwamba huyu ni RPC (kanda wa polisi wa mkoa) alikuwa wapi wakati wale wa Mikindani, Naumbu na maeneo mengine wakitekeleza imani yao hiyo, kama ni sheria iweje ionekane leo baada ya kimbunga hicho kunusa katika maeneo fulani ya vigogo.

KUSINI haitetei shughuli za utoaji uchawi ndani ya jamii kama kweli ni uvunjifu wa sheria, lakini haikubaliani na utendaji kazi wenye uonevu kwa wananchi, yaani hawa wametolewa lakini kundi la watu wengine wanakingiwa kifua kwa kutumia dola. hivi ni serikali gani hiyo inayoamini uchawi? Ni hii ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania au nyingine? Au kuna serikali ya Mtwara inayoamini uchawi?

Kimsingi hii ni imani kama imani zingine, wananchi wamemini kuwa wachawi kwao ni pingamizi la maendeleo na

Mbunge wa Mtwara Mjini, Asnein Murji

ndiyo maana wamekubali kuchanga sh. 2000 kila kaya ili kuwaondoa.

kuna kila sababu ya kujiuliza nyuma ya ukamataji wa waganga kuna nani?

Mbunge wa Mtwara vijiji, Hawa Ghasia

Ama kweli mwaaka mpya mambo mapya

Advertisements