WANAUME WAKATIWA KUFUNGA UZAZI

 

TUNASAIDIA KULEA, NI MKAZI WA WILAYA YA TANDAHIMBA, MKOANI MTWARA

WANAUME nchini wametakiwa kuwa mstari wa mbele kujitokeza kufunga uzazi badala ya utaratibu wa sasa ambapo jukumuhilolimeachwa mikononi mwa wanawake.

Wito huo umetolewa jana na Mratibu wa Uzazi, Baba, Mama na Mtoto wa wilaya ya Tandahimba, mkoani Mtwara, Scholastica Sowani wakati wa maadhimisho ya siku ya unyonyeshaji duniani yaliyofanyika kiwilaya katika kijiji cha Miuta.

Alisema jamii imeweka jukumu la kufunga uzazi kuwa la wanawake, jambo ambalo alisema si sahihi na kwamba wanaume pia wanawajibu wa kufanya hivyo katika jitihada za kufanikisha uzazi wa mpango.

“Sehemu kubwa ya jamii yetu inaamini kuwa wanawake ndiyo wenye wajibu wa kufunga uzazi, nawaomba mtazamo huu ubadilike na sasa wanume wajitokeze zaidi kufunga uzazi ili kufikia malengo ya uzazi wa mpango” alisema Sowani

Alibainisha kuwa kwa kiasi kikubwa huduma za afya ya uzazi zimekuwa zikiachwa mikoni mwa wanawake na hivyo kukwaza malezi bora ya watoto katika familia.

“Mwaka 2008 wajawazito 3389 walipata ushauri na kupima Ukimwi, kati ya hao ni 248 ndiyo ambao waume zao walikubali kupata huduma hizo pia, sawa na asilimia saba, mwaka 2009 wajawazito 5845 walipata huduma za kiliniki na kati yao 463 walikuja na waume zao sawa na asilimia nane, takwimu hizi ni kwa wilaya ya Tandahimba” alisema Sowani

Alifafanua kuwa “Huu ni ushahidi tosha kuwa wanaume wamekuwa mstari wa nyuma katika masuala ya uzazi ndani ya familia, hali hii sio nzuri munapaswa kubadilika…tulee familia zetu pamoja, tushiriki katika huduma za afya pamoja kwa kufanya hivyotutajenga familia bora.

Akizungumzia siku ya unyonyeshaji alisema ni muhimu kwa wazazi kuhakikisha mtoto ananyonya kwa kipindi cha miezi sita ya mwanzo bila ya kumpa chakula kingine ili kumlinda na maradhi yanayoweza jitokeza kwa kumlisha chakula kabla ya umri huo.

Majukumu katika umri mdogo, mkazi wa wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara

“Miezi sita ya mwanzo mtoto anatakiwa anyone maziwa ya mama yake tu, maziwa hayo yanarutuba na yanatosha kwa mahitaji ya mtoto, unapomlisha chakula kabla ya umri huo unaweza kumsababishia maradhi mbalinmbali kwa sababu utumbo wake unakuwa haujakomaa kumeng’enya chakula’ alionya mratibu huyo.

Naye diwani wa kata ya Dinduma wilayani humo, Fadina Mnamande aliwataka wanaume kubadili mitazamo kandamizi ambayo inampa mwanamke jukumu la kulea mtoto.

“Mimba inapatikana kwa ushirikiano wa mwanamke na mwanaume, iweje kulea mtoto aachiwe mwanamke? Naomba wanaume tusaidiane kulea watoto wetu na kushirikia katika huduma za afya, kwa kufanya hivyo itakuwa rahisi kumwacha mtoto anyone kwa miezi sita kabla ya kumpatioa chakula kingine” alisema Mnamande

Aliongeza kuwa “kinyumecho ni vigumu kwa kuwa mama atalazimika kufanya kazi nyingi, jambo ambalo litapunguza uwezo wa kutoa maziwa yanayomtosheleza mtoto…mtoto ataanza kulia njaa kwa kuwa maziwa ya mama hayakumtosha, katika mzingira hayo mama anaamua kumpikia uji mwepesi, hapo tatizo huzaliwa”

mwisho

Advertisements