PAJA LA KUKU OYEEEE!!

“Paja la Kuku oyeee!!” alinukuliwa Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Pro. Jumanne Maghembe alipokaribishwa ‘Msosi’ baada ya kikao kirefu cha Wakulima kule wilayani Mbozi mkoani Mbeya.

Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Mhe: Jumanne MaghembeMapaja ya Kuku, yakiwa tayari kuliwaMapaja ya Kuku

Maghembe baada ya kushusha paja la kuku kwenye sahani ya ‘Mpunga’ yeye na wafuasi wake waliondoka bila ya kula, yaani walisusa ‘Msosi’.

Kauli hiyo ya Waziri inadaiwa kuchagizwa na kauli ya mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Mbozi, kumweleza Maghembe kuwa “Chama legelege huzaa Serikali legelege, Serikali legelege huteua  Mawaziri legelege na wewe ni mmoja wao” alisema mwenyekiti huyo.

Mapaja ya Kuku

Habari zinaeleza kuwa Waziri Maghembe alikwenda wilayani hapo kufuatia kuwapo kwa mvurugano juu ya soko la Kahawa, ambapo katika kikao hicho alitajaria kuongea na wakulima ili kubaini tatizo na hatimaye kulipatia ufumbuzi, lakini kinyumecho aliongea na viongozi wa chama na Serikali wa wilaya hiyo.

Haikuweza kufahamika mara moja sababu ya wakulima hao kutohusishwa kwenye kikao hicho, vuta nikuvute iliibuka na kusababisha viongozi hao kutokwa na busara na hatimaye kurushiana maneno na vijembe vya ‘Kihuni’

Mwisho

Advertisements