MTWARA-BEI YA VYAKULA JUU

HALI ya mfumko wa bei kwa baadhi ya masoko ya bidhaa ya vyakula Dar es Salaam unazidi kushika kasi, huku ukisababisha ugumu wa maisha kwa wananchi.

Vyakula sokoni

KUSINI ilitembelea soko ya Buguruni, Tandika na Tandale na kukuta hali ya mfumko wa bei ikiendelea kupanda.

Vyakula sokoni

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wafanyabishara walisema hali inakoelekea itakuwa ni mbaya kwa wananchi kumudu gharama za maisha.Katika soko kiyangu, Juma Aridi alisema hivi sasa hali inazidi kuwa mbaya kwa bei ya vyakula, kwani bei hizo zinaongezeka kila siku.

“Bei za vyakula, bidhaa kama mafuta, nishati, usafiri na kila kitu zimepaa maradufu, hivyo hata hapa usishangae ndiyo nchi yetu inavyokwenda,” alisema Aridi.

Aridi alifafanua kuwa kilo ya sukari imefikia Sh2,500 kutoka Sh1,000, mchele unauzwa Sh2,500 kwa kilo kutoka Sh800.
Katika soko kuu, Issa Athuman, alisema bidhaa za vyakula zimepanda kutokana na gharama kubwa ya usafirishaji na ongezeko la bei umeme.

Athuman alisema mchele huuzwa kwa  Sh2,500 hadi  Sh2,600 kwa kilo, huku unga Sh900 hadi Sh1,000 kwa kilo, nyanya Sh6,000 kwa plastiki yenye ujazo wa lita tano na viazi Sh5,000 hadi 6,000 kwa kwa ujazo huohuo.

vyakula sokoni


“Sisi tunauza nyanya moja  Sh150 hadi Sh200 na fungu tunapanga kuanzia Sh500 na viazi vitatu tunauza Sh300 hadi Sh500, wakati  mchele tunauza kwa kilo Sh2,400 hadi Sh2,500,”alisema Athuman.

Vyakula sokoni

Alisema bidhaa zingine kama sukari huuzwa kwa Sh2,400 hadi Sh2,500, mafuta ya kula lita moja Sh2600 hadi Sh2,700 na maharagwe yanauzwa kwa Sh2,400 kwa kilo.

 Mwisho