SERIKALI-TUTAPELEKA DAR GESI YA MTWARA

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hawa Ghasia amesema uwamuzi wa Serikali wa kupeleka Dar es Salaam gesi inayochimbwa mkoani Mtwara hauna athari kwa maendeleo ya mkoa huo.

Waziri hawa Ghasia

Ghasia alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki alipokuwa akifungua mkutano wa waandishi na waadau wa habari mkoani humo, uliolenga kutathimini utendaji kazi wa sekta ya habari, mkutano ambao uliandaliwa na Klabu ya Waandishi wa Habari Mtwara (MTPC).

Wachimbaji gesi wakiwa bandari ya Mtwara

Alisema uwamuzi huo wa Serikali utauwezesha mkoa wa Mtwara kupiga hatua za kimaendeleo kwa kuvutia wawekezaji ambao watakuza sekta ya ajira kwa wananchi na hivyo kuondoa umasikini wa kipato unaowakabili.

Waziri huyo ametoa msimamo huo wa Serikali siku chache baada ya Chama cha Wananchi (Cuf) mkoani hapa kutangaza kuitisha maandamano makubwa kupinga uwamuzi wa Serijkali wa kujenga bomba litakalosafirisha gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam na maeneo mengine ya nchi.

“Kwanza wananchi watambue kuwa ile gesi itakuwa haigaiwi bure, utalazimika kununua kama vilivyo kwa bidhaa zingine, pili Serikali imesema inalenga kuongeza uzalishaji wa umeme kwa megawati 300 kutokana na gesi ya Mtwara, hivyo basi ni lazima gesi isafirishwe hadi kwenye machine za kuzalisha umeme” alisema Ghasia

Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja akiwasilisha Mswada wa ujenzi wa bomba na gesi kutoka Mtwara hadi dar es Salaam, bungeni Dodoma

Alifafanua kuwa “Tukisema tuchukue majenereta ya Ubongo yaje kufungwa Mtwara sisi tutafaidika nini na mitambo hiyo zaidi ya kuzalisha moshi na joto…hata Saud Arabia wangekataa kuuza mafuta yao kwa nchi zingine wangeendelea kuwa masikini…

Mimi ndiyo mbunge wa Mtwara Vijijini na gesi inayotajwa ipo jimboni kwanu kama ningeona kuwa uwamuzi huo wa Serikali hauna maslahi kwa wananchi wangu ningekuwa wa kwanza kupinga…nawahakikishia kuwa gesi ile itawanufaisha wananchi wa Mtwara” alisema waziri huyo

Ghasia alivitaka vyombo vya habari mkoani humo kutumia fursa waliyonayo kuelimisha wananchi juu ya masuala ya maendeleo na kuhakikisha wanafanya kazi kwa kutanguliza masilahi ya umma.

Awali Katibu Mkuu Mtendaji MTPC, Rashidi Mussa alisema mkutano huo umelenga kujadili mafanikio na changamoto zinazoikabili sekta bya habari mkoani humo ili kuandaa mzingira bora ya etendaji kazi wa waandishi wa habari.

“Kwa ufadhili wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), tumeweza kuitisha mkutano huu wa wadau ili kwa pamoja tutathimini sekta ta habari mkoani hapa, tukosoane na tupongezane” alisema Mussa

Mwisho

Advertisements