KOROSHO ZAENDELEA KUWATESA WAKULIMA MTWARA

WAKULIMA wa vyama Saba vya msingi vya ushirika wa kilimo na masoko vya

Hili ndilo zao la Korosho linalotesa wakulima Mtwara

wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara, wanaendelea kuteseka kwa kukosa malipo ya kwanza ya mauzo ya korosho, kinyume na utaratibu uliotangazwa na Serikali.

Serikali kupitia Bodi ya Korosho Tanzania (Cbt) ilitangaza kuwa wakulima watalipwa asilimia 70 ya dira ya bei ya korosho kama malipo ya awali mara wanapouza korosho zao katika vyama vya msingi kabla ya malipo ya asilimia 30 yanayofanyika baada ya korosho hizo kuuzwa kwa wanunuzi wakubwa.

Msimu 2011/12 Serikali ilitangaza dira bei kuwa ni sh. 1200 kwa kilo ya korosho na kwamba wakulima watalipwa asilimia 70 ya bei ambayo sawa na sh. 850 kama malipo ya awali, hata hivyo mambo yamekwenda kinyume baada ya vyama Saba kushindwa kutekeleza agizo hilo hadi sasa.

Korosho baada ya kuvunwa

Meneja Mkuu wa Chama Kikuu cha Ushirika Tandahimba, Newala (Tanecu) Daimu Mpakate alikiambia kiao cha Baraza la Madiwani wa Tandahimba mwishoni mwa wiki kuwa vyama hivyo vimeshindwa kulipa malipo ya awali kutokana na kuyumba kwa soko la korosho.

“Hali ya soko la korosho si nzuri, kati ya vyama 71 vya wilaya ya Tandahimba, vyama Saba hadi sasa havijalipa malipo ya awali, vyama vyote 71 havijalipa malipo ya pili kama ilivyozoeleka katika misimu iliyopita kuwa wakati kama huu wakulima wangekuwa wanasubiri malipo ya tatu” alisema Mpakate

Alifafanua kuwa “Katika kuhakikisha wakulima hawa wa vyama Saba wanapata malipo yao ya awali tumeviomba vyama 22 kuongeza ukomo wa madeni wa sh. 4.5 bilioni ili kuviwezesha kukopa fedha za ziada benki”

Alibainisha kuwa hadi sasa kilo 45,479,465 za korosho zimekusanywa kutoka kwa wakulima ambapo kilo 21,401980 zimeuzwa kwa wanunuzi wakubwa sawa na asilimia 47 na kilo 24,077,485 sawa na asilimia 53 hazijauzwa na zimeendela kuhifadhiwa katika maghala.

Mwenyekiti wa Tanecu, Yusuf Nannila alisema kuwa jitihada mbalimbali zinafanywa na chama chake kuhakikisha wanapata ufumbuzi wa kuyumba kwa soko la korosho ikiwa pamoja kuuza korosho kwa njia ya mtandao wa kompyuta (Internet)

Nabangua korosho

“Hivi karibuni tutaanza kuuza koroho nje ya nchi kwa kutumia mtandao (internet), ofisa masoko wetu alikuwa masomoni Uganda, na hivi karibuni atarejea kuhakikisha tutaondokana na tatizo hili, ili wakulima wetu wasizidi kuathirika…naomba tuendelee kuwa na subira kwani si tatizo la Mtwara, ni tatizo la korosho Tanzania” alisema Nannila

Mkuu wa wilaya hiyo, Hasna Mwilima alitumia fursa kuwataka wananchi kuondoa hofu juu ya upatikanaji wa malipo ya pili kwa kusisistiza kuwa Serikali inalifanyia kazi suala hilo.

Mhe. Rais hii ndiyo Korosho Unatusaidiaje?

“Waambieni wakulima wasiwe na wasiwasi juu ya malipo ya pili, ni lazima watayapata…Serikali kwa sasa inalishughulikia suala hili…tunafahamu kuwa watoto wetu wahajaenda shule kutokana na hali hii, nitafanya kikao na wakuu wa shule ili kuwaruhusu wanafunzi kuanza shule hata kama hawajatimiza mahitaji yote ya shule” alisema Mwilima

Mwisho

Advertisements