HATIMAYE SERIKALI YANYWEA, WANAFUNZI NDANDA WAREJESHWA

HATIMAYE Serikali imetoa tamko rasmi la kuwarejesha wanafunzi 20 waliofukuzwa shule ya sekondari Ndanda wilayani Masasi mkoani Mtwara kwa sababu za kidini.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Joseph Simbakalia

Wanafunzi hao waisilamu walifukuzwa shule 21 Desemba mwaka jana kufuatia madi ya kujengwa kwa msikiti shuleni hapo na kuushtumu uongozi wa shule hiyo kupandikiza vimelea vya udini  kwa wanafunzi hao.

Kwa mujibu wa tamko hilo la serikali lililosainiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Mstaafu Joseph Simbakali, katika kikao cha Januari 31, mwaka huu kilichofanyika mjini Mtwara serikali iliridhia kuwarejesha wanafunzi hao shuleni bila masharti.

Kinyume na alivyonukuliwa asubuhi katika mahojiano na TBC, Simbakali alisema kuwa ni wanafunzi Watatu tu ndiyo walikidhi vigezo na masharti ya kurejea shuleni.

Kauli hiyo ya Simbakalia ilifuatiwa na mwitikio hasi kutoka kwa waisilamu, waliopanga kufanya maandamano makubwa shuleni hapo ili kuzuia kufanyika kwa mtihani wa kidato cha sita.

KUSINI inayo nakala ya tamko hilo, na inatumia fursa hii kuipongeza serikali kwa kuzima mgogoro wa kidini ambao ulikuwa hatari kwa taifa letu