MGOGORO WA KIDINI NDANDA WACHUKUA SURA MPYA

MGOGORO wa kidini uliosababisha wanafunzi 20 kufukuzwa shule ya sekondari ya wavulana Ndanda, (Ndanda High School) wilayani Masasi mkoani Mtwara  umechukua sura mpya baada ya agizo la serikali la kutaka wanafunzi hao kurejeshwa shuleni kugonga mwamba.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Mstaafu, Joseph Simbakali

Naibu waziri Tamisemi anayeshughulikia Elimu, Kassim Majaliwa

Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Joseph Simbakalia akihojiwa na TBC leo (Febuari, 6, 2012) alisema ni wanafunzi watatu tu waliorejeshwa shuleni ambao rufaa zao zilisikilizwa.

Ni kweli serikali iliagiza kurejeshwa kwa wanafunzi hao kwa kufuata utaratibu ambao ulitaka wazai kukata rufaa na kuniletea kwa ajili ya kusikilizwa upya madai yao kasha kutengua maamuzi…ni wanafunzi watatu tu waliofanya hivyo” alisema Simbakalia

Alifafanua kuwa “wengine hawataruhusiwa kufanya mitihani au kurejea darasanai kwa sababu hawakufuata masharti”

Serikali kupitia Naibu Waziri wa Tamisemi anayeshughulikia elimu, Kassim Majaliwa aliagizwa uongozi wa mkoa kurejesha shuleni wanafunzi hao, hatua hiyo ilitokana na waziri huyo kupata maenelezo ya kina kutoka kwa uongozi wa shule na wanafuni juu ya mzozo hu.

Mufti wa Tanzania Shabaan Simba akiteta jambo na Rais Jakaya Kikwete

Kufuatia kauli hiyo ya Simbakali kituo cha redio cha Imani kilichopo mjini Morogoro, kimetangaza maandamano makubwa kupinga kufanyika kwa mitihani ya kidato cha sita shuleni hapo kabla ya kurejeshwa kwa wanafunzi hao.

 

Baadhi ya wanafunzi wa Ndanda High School

Katika kipindi cha redio hiyo asubuhi ya Februari 6, 2012 mtangazaji wa kipindi hicho amesikika akihamasisha waislamu kote nchini kuungana na kupinga hatua hiyo, na kwamba viongozi mbalimbali wa dini hiyo watakusanyika mjini Ndanda wilayani Masasi mkoani Mtwara Februari 8 mwaka huu kwa maandamano

mwisho

Advertisements