CUF; GESI KUIGEUZA MTWARA KUWA ‘SUDAN YA KUSINI’

CHAMA cha Wananchi (CUF) Manispaa ya Mtwara Mikindani, kimeitaka serikali kutengua uwamuzi wake wa kusafirisha gesi ya Mtwara kwenda Dar es Salaam na maeneo mengine ya nchi, na kutaadharisha kuwa vinginevyo eneo hilo litageuka kuwa ‘Sudani Kusini’.

Kisima cha Gesi

Waziri wa Nishati na Madini, william Ngeleja

Chama hicho kimesema kipo tayari kuendesha hujuma dhidi ya mradi wa ujenzi wa bomba la gesi ili kuhakikisha rasilimali hiyo haisafirishwi nje ya mkoa ikiwa mbichi.

Sudani Kusini ni nchi changa ambayo imejitenga kutoka nchi ya Suadani Kasikazini kutokana na Sudani Kusini kupinga usafirishaji wa mafuta kutoka eneo hilo na kwenda sehemu zingine za nchi, hali iliyosababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Uwamuzi huo umetangazwa jana na Diwani wa Kata ya Chikongola wilayani Tandahimba, mkoani Mtwara, Makuyega Makuyega alipokuwa akihutubia mkutano wa adhara eneo la Kokobichi mjini Mtwara na kusisitiza kuwa  wapo tayari kwa vurugu kama ilivyotokea Sudani Kusini.

Makuyega ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mkutano huo alisema kuwa wakati umefika kwa wananchi kuhakikisha wanashikamana na kudai haki yao kwa madai gesi hiyo imetokana na kudra za Mungu kwa ajili ya ya kuwanufaisha wananchi wa Mtwara.

“Wananchi wa Mtwara hamtakiwi kuogopa serikali, tushikamane kuhakikisha kwamba tunadai haki yetu, na haki yetu kamwe haiwezi kuchukuliwa hivi hivi, tuige mfano wa Sudan ya Kusini, ambao walichoshwa na uporwaji wa mafuta na wakaamua kwa pamoja na wameweza kufanikisha ” alisema Makuyega

Mwenyekiti wa CUF, Taifa Ibrahim Lipumba

Aliongeza kuwa “Hamtakiwi kuogopa,  vijana songeni mbele kuhakikisha gesi yetu haiendi popote, msiogope vitisho  vya serikali mkiendelea kuogopa tutaonewa na serikali, na haki yetu itachukuliwa…tunaiomba serikali ibadili uwamuzi wake vingnevyo Mtwara itakuwa Sudan ya Kusini ya Tanzania”

Alihoji kuwa endapo  lengo la serikali  ni kuonyesha umoja na mshikamano baina ya wananchi wa kusini mwa Tanzania  na wananchi wa Kaskazini,  lini dhahabu ya Shinyanga italetwa Mtwara?
Awali katibu wa CUF Manispaa ya Mtwara Mikindani Saidi  Kulaga alisema wakazi wa mkoa wa Mtwara wanayo kila sababu ya kupinga gesi kusafirishwa hadi pale uwekezaji utakapojitosheleza mkoani humo.

“Leo wawekezaji wanakimbilia Mtwara kwa sababu ya upatikanaji wa umeme wa uhakika na uwapo wa gesi ya uhakika, sasa unaposafirisha kwenda Dar es Salaam unataka wawekezaji waje Mtwara kwa lipi…gesi ambayo ingewaleta huku wataipata hukohuko…tunasema gesi haiendi Dar ng’o” alisisitiza Kulaga.

“Kama wanataka kusafirisha, wasafirishe bidhaa zinazotokana na gesi hiyo, sio gesi mbichi….gesi isafishwe hapa kasha iende kokote kuuzwa na si kuisafirisha mbichi”

CUF kupitia mikutano yake ya amsha, amsha imetangaza kuandaaa maandamano makubwa kupinga uwamzi wa serikali wa kusafirisha gesi kutoka Mtwara na kwenda maeneo mengine ya nchi.

Tayari Mbunge wa Mtwara Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menenjimenti ya Utumishi wa Umma, Hawa Ghasia alitetea uwamzi wa serikali kwa madai utaendelea kulinda maslahi ya wakazi wa Mtwara.

Mwisho
 

Advertisements