VITA YA AL-SHABAB NA KENYA YAPUNGUZA WAHAMIAJI HARAMU MTWARA

Wahamiaji Haramu (Wasomali) wakiwa Mahakamani mkoani Mtwara

VITA baina ya Kenya na kundi la Al-Shabab nchini Somalia vimesababisha kupungua kwa wahamiaji haramu wanaoingia mkoani Mtwara. Imebainishwa

Kaimu Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Mtwara, Hamidu Mkambala amesema kwa sasa idadi ya wahamiaji haramu wanaokamatwa mkoani humo imepungua tangu kuanza kwa vita hivyo ikilingwanishwa na kipindi cha nyuma.

“Kabla ya hapo tulikuwa tunakamata hadi wahamiaji haramu 100 kwa siku, lakini siku za hivi karibuni idadi hiyo imepungua…mfano mwaka huu ni wahamiaji haramu 11 tu tuliowakamata” alisema Mkambala

Aliongeza kuwa “Unajua Kenya wameimarisha mipaka yao baada ya kuingia vitani na Al-Shabab hasa pwani ya bahari ya Hindi ambako wahamiaji hao walikuwa wanapakiwa kwenye majahazi na kuteremshwa Mtwara”

Ofisa huyo alibainisha kuwa mbali na hiyo, askari wake wamefanikiwa kuvunja mtando wa usafirishaji wa wahamiaji hao kwa kuwakamata watu wanne ambao walikuwa wanawapokea na kuwapa hifadhi ya muda.

“Kesi zipo Mahakamani, ila moja ya sababu ya kupungua kwa idadi ya wahamiaji haramu mkoani hapa ni pamoja na kuvurugwa kwa mtandao wao” alieleza ofisa huyo

Alitoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa askari uhamiaji mkoani hapa ili kuwabaini watu wanaojihusisha na biashara ya kuwasafirisha wahamiaji hao, ambao alieleza kuwa ni hatari kwa usalama wa nchi.

mwisho