JAPAN YAPIGA JEKI POLISI MTWARA

Kituo cha zamani cha polisi katika kijiji cha Kilambo, mkoani Mtwara, Mpakani mwa Tanzania na Msumbiji. Tangu mwaka 1964 polisi wamekuwa wakitumia nyumba hii ya mkazi kijijini hapo kama kituo.

SERIKALI ya Japan kupitia shirika la Kimataifa linashughulikia wahamiaji (IOM) imetoa msaada wa magari matatu, boti na kituo cha polisi kwa jeshi la polisi na uhamiaji mkoani Mtwara ili kuweza kukabili wahamiaji haramu na maharamia.

Akikabidhi akikabodhi msaada huo Balozi wa Japan Nchini, Masaki Okada alisema serikali yake imechangia kiasi cha dola za kimarekan 2.4 milioni sawa na sh. 3.6 bilioni za Kitanzania kwa IOM ili kusaidia utekjelezaji wa misaada mbalimbali ya kibinadamu inayowahusu wahamiaji.

Alisema tayari ameshuhudia shirika hilo likikabidhi magari 11 na boti 3 kwa polisi na uhamiaji katika maeneo mengine ya nchi ambayo yapo mipakani kwa lengo la kuimarisha mipaka , hivyo ni matumaini yake kuwa vyombo hivyo vitatumika kwa malengo kusudiwa.

“ Nina amini kuwa kituo hiki cha polisi kwa hakika kitachangia juhudi za Serikali ya Tanzania katika kuimarisha, kuongoza na kudhibiti mipaka…ni matarajio yangu kuwa majengo na magari yatatumika kikamilifu na kutuzwa vizuri ili yaweze kudumu kwa muda mrefu” alisema Okada

Balozi wa Japan Nchini, Masaki Okada, katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Mbarak Abdulwakil na kushoto ni Mkuu wa Shirika la Kimataifa linaloshughulikia wahamiaji (IOM), Damien Thuriaux. Halfa hiyo ilifanyika jana kijiji cha Kilambo mpakani mwa Tanzania na

Akipokea msaada huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Mbarak Abdulwakil aliishukuru Japan na IOM kwa msaada wa magari matatu aina ya Toyota Land Cruser, boti na kituo kwa polisi na  ukarabati wa ofisi ya uhamiaji zilizopo Kilambo mpakani mwa Msumbiji na Tanzania.

Alisema msaada huo umefika wakati muafaka ambapo Mtwara imekuwa ikikabiliwa na tatizo la wahamiaji haramu na tishio la maharamia, hivyo unaweza kuwa chachu ya kukabiliana na vitendo hivyo.

Kituo kipya cha polisi kilichojengwa Kilambo kwa msaada wa Japan

“Tunayo matatizo ya Wahamiaji haramu, Maharamia na Wavuvi haramu, msaada huu wote umelenga katika kukabiliana na vitendo hivyo…waliongea awali yangu walisema wanawaomba muvitunze, mimi nawaagiza muvitumie vifaa hivi kwa kazi iliyokusudiwa na kuvitunza kwa uwangalifu” alisema Abdulwakil

Aliongeza kuwa “Tunashukuru sana Japan na OIM kwa kufanikisha msaada huu, ni imani yangu wananchi wa Kilambo wamefurahishwa nayo kwani umewaongezea chachu katika suala nzima za ulinzi wa mpaka wetu”

Kwa upande wake mkuu wa IOM Tanzania, Damien Thuriaux alisema shirika lange haliungi mkono wahamiaji haramu lakini linatoa msaad wa kibinadamu kwao hususani kuwarejea makwao kwa hiyari.

“Katika kipindi cha 2009-2011 jumla ya wahamiaji haramu 4939 ambao walikuwa magerezani nchini Tanzania walirejeshwa kwao kupitia shirika letu kwa msaada wa Japan, wengi wa wahamiaji hao walikuwa Waethiopia na Somalia…tunaamini iwapo mipaka itadhibitiwa idadi ya wahamiaji ha itapungua” alisema Thuriaux

Mwisho

 

 

Advertisements