MTWARA WAKUNWA NA UTEUZI WA TIDO

Mkurugenzi Mtendaji Mpya wa Mwananchi Communications Ltd (MCL) Tindo Mhando

WASOMAJI na wapenzi wa Magazeti ya Mwananchi Communications Ltd (MCL) mjini Mtwara wamempongeza Mkurugenzi Mtendaji mpya wa kampuni hiyo Tido Mhando kwa kuteuliwa kwake kushika wadhifa huo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na KUSINI jana , wasomaji hao walisema wanaupongeza uongozi wa MCL kwa kumteua Mhando kushika usukani wa kuendesha kampuni hiyo, ambapo pia walimpongeza mhando mwenyewe kwa kutwaa nafasi hiyo.

Walisema wao kama wasomaji na wapenzi wa magazeti ya MCL (Mwananchi, Mwananchi Jumapili, The Citizen, The Citizen on Sunday na Mwanaspoti) wamefarika na uteuzi huo na kwamba ni imani yao kuwa Watanzania wataendelea kupata habari za kweli zinazozitangia uweledi na hivyo kuwa kichocheo cha maendeleo.

“Nimekuwa mpenzi wa gazeti la Mwananchi baada ya kuridhishwa na habari zinazochapiswa, habari hizo ni za ukweli na zisizoegemea upande wowote, wamesimama kwenye ukweli” alisema Hassan Issa

Aliongeza kuwa “Sote tunafahamu utendaji kazi wake mahiri pale alipokuwa TBC, kabla yake watu walikuwa hawaangalii TBC alipokuja yeye kila mtu alitaka kupata habari kupitia television hiyo…leo amehamia Mwananchi ni imani yangu Mwananchi itakuwa juu zaidi’

Msomaji mwingine aliyejitambulisha kwa jina Jamadi Maulid huku akiwa ameshikia gazeti la The Citizen mkononi alisema “Nampongeza sana Tindo kwa kuteuliwa kwake kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi…naupongeza sana uongozi wa Mwananchi kwa kumteua Tindo”

Sadick Saidi alisema amekunwa na uteuzi huo kwa madai kuwa utaongeza uhuru wa habari na kujieleza kwa wananchi hivyo kupaza sauti zao.

“Sauti za wanyonge zinahitaji kusikika…tatizo vyombo vingi vya habari havitoi nafasi, nina imani na Tindo kuwa sasa mwananchi itakuwa gazeti la kupaza sauti za wanyonge”

 

 

Advertisements