VURUGU TANDAHIMBA

HALI ya usalama wilaya ya Tandahimba, mkoani Mtwara imeendela kuwa

Watembea kwa miguu wakijaribu kupita eneo lililowekwa magogo
kuziba barabara kuu itokayo Tandahimba, kwenda Newala katika eneo la
kijiji cha Dinduma.

tete, kufuatia baadhi ya wakulima wa korosho wilayani humo kufanya

vurugu wakishinikiza Serikali iwalipe malipo ya pili ya mauzo ya zao

hilo.

 

Wakulima hao wanadaiwa kuamrisha kufungwa kwa shule ya sekondari na

msingi za msingi za kijiji cha Mihambwe na kuwachapa bakora walimu,

kabla ya kuvamia kituo kidogo cha polisi kijijini hapo na kutembeza

mkong’oto kwa polisi wawili waliokuwapo kituoni hapo.

 

Kwa mujibu wa mkuu wa shule ya sekondari Mihambwe, Kapinga Innocent

shule zilizokumbwa na mkasa huo ni shule ya sekondari Mihambwe, shule

za msingiRuvumana Mihambwe.

 

Polisi wakiwa katika doria wilayani Tandahimba, mkoani Mtwara

Tukiohilolilitokea Aprili 12, mwaka huu ambapo askari PC Almasi

alijeruhiwa vibaya na kulazwa hospitali ya wilaya Tandahimba, kwa

mujibu wa muuguzi wa zamu wodi namba tatu, Helena Mshana askari huyo

anaendelea vizuri na matibabu.

 

Aprili 13, mwaka huu wakulima hao pia wanadaiwa kufunga barabara kuu

ya Mtwara, Tandahimba hadi Newala kwa kuagushia miti mikubwa

barabarani, kuweka magogo, kuchimba mifereji  barabarani na

kusababisha kukosekana kwa mawasiliano ya barabara kwa siku mbili

mfululizo.

 

Hali ya mji wa Tandahimba imekuwa tulivu ambapo maeneo ya sokoni na

madukani hakuna huduma yoyote inayotolewa, isipokuwa baa ya polisi

ambako huduma ya chakula inapatikana, huku wakazi wake wakidaiwa

kukimbilia porini kujificha.

 

Aidha wakulima hao waliangusha na kuchoma moto nguzo za umeme zaidi ya

Waandishi wa habari wakijaribu kutoa magogo yaliyofunga
barabara kuu itokayo Tandahimba hadi Newala katika eneo la kijiji cha
Nahyanga

10 katika vijiji vya Malamba, Miule, Mahuta na Matogoro hivyo

kusababisha kukosekana kwa nisharti ya umeme katika miji ya

Tandahimba, Nahyanga na Mahuta.

 

Wakizungumza na waandishi wa habari kwa sharti la kutotajwa majina

baadhi ya wananchi hao walisema wameamua kufanya vurugu hizo ili

kufikisha kwa urahisi kilio chao cha kutaka walipwe fedha zao za mauzo

ya korosho kwa serikali.

 

“Tunachotaka malipo ya pili, hawa jamaa wamezoea kutunyonya kweli,

toka kipindi kirefu…leo hii tumechoka kabisa, tunataka serikali kuu

wajue” alisema mkulima huyo wa kijiji cha Malamba

 

Jitihada za polisi kurejesha mawasilino ya barabara zimegeuka mithili

ya mchezo wa kuigiza pale walioyaondoa magogo na miti na muda mfupi

baada ya wao kupita wananchi waliziba tena kwa miti mikubwa zaidi ya

awali.

 

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Mtwara, Focas Malengo amethibitisha

kutokea kwa tukiohilona kuongeza kuwa zaidi ya watu 50 wamekamatwa

wakihusishwa kuhusika na tukiohilo.

 

Alisema kuwa wakulima hao pia walivunja na kuporamalikatika nyumba

za askari polisi Wanane na watumishi wawili wa halmashauri ya wilaya

hiyo, ambapo pia walipiga mawe gari ya Takukuru wilayahi humo na

kuvunja kioo cha mbele.

 

“Walivamia nyumbani kwa Mhandisi Magota, Mwanasheria wa halmashauri

Charles Ndoromo, walivunja nyumba na kuporamalimbalimbali ambazo

thamani yake haijajulikana mara moja” alisema Malengo

 

Aliongeza kuwa “Vurugu hizo pia zilisababisha ofisi ndogo ya Chama

Kikuu cha Ushirika Tandahimba, Newala (Tanecu) ilivunjwa na kupora

vifaa mbalimbali ikiwemo Kompyuta, pia ofisi za chama cha walimu

zilivamiwa na kuibiwa Kompyuta mbili …kimsingi hali si shwari, ila

jeshi langu linaendelea kurejesha amani”

 

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akijibu swali bungeni Alhamisi hii alisema

tayari upembuzi wa malipo ya wakulima wa korosho umekamilika tayari

kwa kukabidhiwa kwa Gavana wa Benki Kuu.

 

Chini ya mfumo wa stakabadhi ghalani bei dira ya korosho msimu huu ni

sh. 1200 ambapo wakulima walilipwa sh. 850 sawa na asilimia 70 na

wanadai sh. 350 sawa na asilimia 30 ya dira ya bei.

Mwisho

Advertisements