SHIBUDA MAMLUKI CHADEMA?

Kwa kila ninavyojaribu kufikiri, jibu linakuja kuwa John Shibunda Mbugge wa Maswa, ni CCM aliyeingia Chadema kwa lengo la kukivuruga chama hicho, itakumbukwa kuwa hiyo ni mara ya nne Shibuda anakiingiza Chadema kwenye mgongano.

1. Kupinga msimamo  wa Chadema wa kutotambua mchakato matokeo ya kura uliomrejesha JK madarakani mwaka 2005

2. Alipinga msimamo wa chama hicho wa kukataa kuongezwa kwa posho

3. Alikwenda kwenye hafla iliyoandaliwa na Kj kule dodoma baada ya kulihutubia Bunge

4. Ametangaza akiwa na wana CCM kugombea urais mwaka 2010 kupitia Chadema

Ukweli simuelewi Shibuda ana nini moyoni mwake, mimi sio mfuasi wala mwananchama wa Chadema ila mkereketwa na siasa vyama vingi kwani ndiyo msingi wa demokrasia huru….huwa najiuliza iwapo Chadema itaparaganyika kwa mbinu za Shibuda nani atakuwa mpinzani?

Advertisements