KATIBA IMALIZE KASORO ZA MUUNGANO

Moja ya Kanisa lililoharibiwa na vurugu za Wazanzibar wanaodai kupinga Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

Chokochoko za Wazanzibar kudai kile wanachokiamini kuwa ni Taifa huru kwa maana lisilo ungana na jingine zilianza mbali na sasa limefikia hatua mbaya ya kuvunjika kwa amani yetu.

Zanzibar ambayo ilijulikana kama kisiwa cha amani kimegeuka kisiwa cha damu moto na vurugu, hili halikubaliki.

Moto barabarani Zanzibar

KwaMtazamo wa KUSINi ni kwamba katika hili linaweza kumalizwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano Watanzania kwa aidha kuwa na serikali tatu yaani Tanganyika, Zanzibra na ile ya Muungano au Kuifuta Zanzibar na kubaki na Tanzania bara na visiwani.

Tatizo hapa ni kwamba kwa Zanzibar kuendelea kutambulika kamanchi ndani ya muungano inawafanya Wazanzibar waone wao ni muhimu zaidi ya Watanganyika ambao waliiua nchi yao na kuzzalisha Tanzania

Advertisements