WATOTO WENYE ULEMAVU WA AKILI SIO MZIGO KWA JAMII

Watoto wenye ulemavu wa akili wa shule ya msingi Mji Mpya wilayani tandahimba, mkoani Mtwara wakiimba wimbo wa Taifa

Wanafunzi hao wakiwa darasani wanajifunza

Wanavuna mahidni katika shamba lao

wameshavuna tayari

Kumekuwapo na imani potofu kuwa watoto wenye ulemavu wa akili ni mzigo katika jamii kwa maana hawawezi kujitegemea.

 Kutokana na imani hiyo watoto wengi wamekuwa wakikosa fursa ya kupata haki yao ya msingi ya elimu, wazazi au walezi wengi wamekuwa wakikataa kuwekeza katika elimu kwa ajili ya watoto wao wenye ulemavu wa akili kwa mdai kuwa hata kama wakisoma hawana uwezo wa kuajiriwa popote. Picha hizi zilizopigwa na KUSINI zinaonesha kuwa watoto hao wanauwezo wa kujifunza na kuwa jengea uwezo wa kujitegemea katika kuendesha maisha yao kama tunavyowaona katika picha. Kwa mujibu wa mwalimu mkuu wa shule ya watoto wenye mahitaji maalum ya Mji Mpya wilayani Tandahimba, mkoani Mtwara, Mohamedi Chipuputa watoto hao wanaweza kujivunza na kuweza kujiendehsea maisha yao katika fani mbalimbali za ufundi, licha ya kukiri kuwa ni gharama kuwaelimisha. Chipuputa anasema jitihada kubwa zinahitajika kw serikali na wadau wa elimu kuhakikisha shule hizo zinajengwa kila kata ili kuwawezesha watoto wengi wenye matatizo ya akili ambao wamefungiwa ndani kupata fursa ya elimu ili waweze kujiajiri katika fani mbalimbali za ufundi zikiwemo, ushonaji nguo, na seremalaMWISHO

Advertisements