Safari ya Gesi Dar yaiva

Watoto wa kijiji cha madimba na vijiji jirani walishuhudia makabidhiano hayo

Makabidhiano ya eneo la kujenga kiwanda cha kusafisha gesi katika kitongoji cha Mchepa kijiji cha Mandimba, Mtwara vijijini mkoani hapa, kunaifanya mchakato wa safari ya kupeleka gesi dar es Salam kuiva.

Makabidhiano hayo yalifanyika Julai,22 mwaka huu kijijini hapo na Waziri wa Nishati na Mdini Prof. Sospita Muhongo kwa kampuni ya kichina ya CPTDC.

Tayari TCCIA, CUF na wananchi mbalimbali walionesha nia ya kupinga mradi huo ambao walisema unapora rasilimali za wanakusini ili hali wenyewe hawajanufaika nayo.