Nane Nane Kanda ya Kusini kwa Maslahi ya nani?

Waziri Ghasia akiangalia baadhi ya bidhaa zilizomo katika maonesho hayo

Maonesho Nane Nane Kanda ya Kusini kanda ya Kusini yamezinduliwa jana (Agosti, 3, 2012) na

Watu katika maonesho

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Hawa Ghasia katika viwanja vya Ngongo Manispaa ya Lindi.

Eneo hili ni eneo la kudumu la maonesho hayo, yaani kila mwaka maonesho hayo yatafanyika katika viwanja hivyo, kwa fafsiri rahisi ni kwamba kwa sasa wilaya hazitaadhimisha tena sikukuu hiyo katika maeneo hayo bali zitalazimika kupeleka bidhaa zao katika viwanja hivyo.

Swala la msingi la kujiuliza ni kwamba haya ni maonesho kwa ajili ya nani? kama wakulima hivi inawezekana wakulima wa nanyumbu, Liwale kutumia nauli zao kwenda kujifunza chochote juu ya kilimo katika viwanja hivyo.

Hapa watawala wanataka kutueleza kuwa watu walio karibu na viwanja hivyo ndiyo wanaopaswa kupata elimu hiyo kwa sababu ndiyo wasiohitaji gharama yeyote kwenda kujifunza, wengine ni wale watakaotambulika na halmshauri huska, watakaolipwa posho ili waende kujifunza…kuna logiki yoyote hapo?

Kama kulikuwa na hoja ya kuwapo kwa maonesho ya kanda kwanini basi kabla ya maonesho hayo yangetanguliwa na maonesho ya kata, wilaya, mkoa na baadae kanda?