Meya Mstaafu Mtwara awania uwenyekiti CCM Manispaa

Chinkawene kushoto akikabidhiwa fomu na katibu wa CCM Manispaa ya Mtwara Mikindani Mkalinga

Aliyekuwa Meya Mstahiki wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani 2005/10Ali Mussa Chinkawene amechukuwa fomu leo (Agosti, 22, 2012) kuwania uwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi manispaa ya Mtwara-Mikindani.

Fomu hiyo amechukua kutoka kwa Katibu waCCM wa manispaa hiyo, Issa Mkalinga huku akitamba kuwa amedhamiria kukinusuru chama hicho kupoteza mwelekeo katika kipindi hiki ambacho alisema vyama “rafiki” vinakuwa na nguvu

“Nataka kumaliza makundi ndani ya chama ili kutoviapa nafasi vyama rafiki kuchukua jimbo” alisema Chinkawene

Kwa mujibu wa Mkalinga watu Sita wamejitokeza kwa kila nafasi inayogombaniwa.

Mwisho

Advertisements