Jitokezeni kuhesabiwa Sensa

Sensa kwa Maendeleo Jiandae Kuhesabiwa

Kesho Agosti, 26 ni siku ya sensa kwa Watanzania, kazi hiyo itaanza saa 6:00 usiku wa leo

Makazi

kuamkia kesho.

Uongozi wa KUSINI unawaomba wananchi wote wajitokeze kuhesabiwa ili kufanikidha adhima ya Serikali yetu ya kupanga mipango kulingana na idadi na mahitaji ya wananchi wake.

Sensa kwa Maendeleo, Jiandae Kuhesabiwa.

Maandalizi  ya Sensa Mtwara yakamilika

MAANDALIZI ya Sensa mkoani Mtwara yamekalika kwa zaidi ya asilimia 95.

Kwa mujibu wa Mratibu wa Sensa ya Watu na Makazi wa Mkoa wa Mtwara, Simon Semindu yatari ofisi yake imepokea kutoka makao makuu na kusambaza vifaa vyote muhimu kwa ajili ya kazi ya kuhesabu  na makazi yao.

“Tumepokea vifaa vyote muhimu na tayari tumevisambaza kwa makarani wa sensa katika wilaya husika…kuna upungufu kidogo wa ‘ordinary bags’ (Begi za kawaida)” alisema Semindu na kuongeza kuwa

“Fedha zote tumetuma kwa kila wilaya…pia fedha kwa ajili ya wenyeviti wa vitongoji nazo zimetumwa…kwa hiyo hatutarajii kusikia tatizo lolote kwa sababu maandalizi yametimia kwa zaidi ya asilimia 95”

Kila la kheri