Zahanati yakosa choo kwa miaka 58

Mfano wa jengo la Zahanati (Siyo hii iliyokosa choo) picha hii kwa hisani ya full shangwe blog.

ZAHANATI ya Nala katika Manispaa ya Dodoma inakabiliwa na ukosefu wa choo, maji na umeme tangu mwaka 1954.

Hali hiyo ilibainika hivi karibuni baada ya wakazi na wagonjwa mbalimbali kulalamikia ukosefu wa huduma hizo katika zahanati hiyo.

Baadhi ya wagonjwa waliozungumza na Tanzania Daima jana, walisema zahanati hiyo inakabiliwa na changamoto hizo kwa muda mrefu sasa, jambo ambalo ni usumbufu kwao.

Hata hivyo, walisema kutokana na ukosefu wa choo pamoja na maji, wajawazito wanapokwenda katika zahanati hiyo wanalazimika kubeba maji na mafuta ya taa kwa ajili ya kupatiwa huduma.

Nao manesi wa zahanati hiyo walisema tatizo la kukosa choo na maji ni la siku nyingi na hakuna ufumbuzi wowote.

Wakizungumza kwa masharti ya kutotajwa majina, walisema kitendo cha zahanati hiyo kukosa umeme kinawasababishia kufanya kazi katika mazingira magumu.

SourceTanzania Daima

Advertisements