Makarani Masasi waishiwa madodoso ya Sensa

Tujitokeze kuhesabiwa

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida baadhi ya makarani wa sense katika wilaya ya Masasi, mkoani Mtwara wamelazimika kupumzika kwa siku tatu mfululizo (kuanzia Agost,27hadi Agost, 29) baada ya kuishiwa madodoso marefu ya kuhesabia watu na makazi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya makarani hao walisema kwa sharti la kutotajwa majina kuwa wameshindwa kuendelea na zoezi la kuhesabu watu baada ya kuishiwa fomu za madodoso hayo.

“Fomu za dodoso ndefu zilikuwa chache, tumeandikisha siku moja tu zikaisha…tupo nyumbanihadi tutakapotaarifiwakuwa zimekuja” alisema mmoja wa karani hao.

Mwenyekiti wa Sensa wa wilaya hiyo, Farida Mgomi ambaye pia ni mkuu wa wilaya amethibitisha kutokea kwa hali hiyona kuongeza kuwa taarifa zilitumwa mkoani kwa ajili ya kushughulikia lakini hadi sasa tatizo hilo halijatatuliwa.

“Ni kweli tatizo hilo lipo na tumeripoti mkoani wamesema kesho (leo) wataleta madodoso hayo…mara yatakapoletwa watapelekewa makarani hao ili waendelee na kazi” alisema Mgomi

Aliongeza kuwa “Kwa mwenendo huu naingiwa na wasiwasi iwapo zoezi hili litafanikiwa kikamilifu katika wilaya yangu”

“Ni mapungufu ya kawaida, hata hivyo zoezi halikusimama, tulikuwa tunatoa sehemu yenye madodoso mengi na kpeleka kule walikoishiwa…. leo asubuhi gari zimetumwa kupeleka madodoso huko Masasi” alisema Simon Semindu Mratibu wa Sensa wa Mkoa wa Mtwara

Mwisho

Advertisements