KESHO NI KESHO UCHAGUZI WAANDISHI MTWARA

ofisi ya klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Mtwara

Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Mtwara (MTPC) inatarajia kufanya uchaguzi wa dharura hapo kesho.

Uchaguzi huo umekuja kufuatia klabu hiyo kupitisha Katiba mpya mapema Mei mwaka huu hivyo kuwailazimu kuwa na viongozi kwa mujibu wa katiba hiyo.

Chini ya usimamizi wa Masau Bwire ,wemyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoani Pwani akisaidiwa na mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habarai mkoani Lindi, Abdullazizi Ahamedi.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa klabu hiyo, Kasim Mikongolo, nafai zinazogombewa ni Uwenyekiti, Makamu mwenyekiti, Katibu Mkuu mtendaji, Katibu Msaidizi, Mwekahazina, Mwekahazina msaidizi na ujumbe wa kamati ya utendaji nafasi nne.

mwisho