Wanahabari Mtwara nao kuandamana

Baadhi ya wahariri na waandishi wa habari wakiandamana kulaani mauaji ya wandishi mwezao, Daudi Mwagosi

Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Mtwara kesho (septemba, 12, 2012) wataandamana kimyakimya kupinga mauaji ya mwandishi wa habari mwenzao Daud Mwangosi aliyeuawa akiwa mikononi mwa polisi.

Mwangosi ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Iringa Press Club aliuawa kwa kulipuliwa na kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu.

Mwenyekiti wa Mtwara Press Club Hassan Simba amesema waandishi wa mkoa wa Mtwara wataungana na wenzao nchini kote kuandamana kupinga mauaji hayo.

Alisema waandishi hao watakuwa wamevalia suti nyeusi ikiwa ni ishara ya maombelezo huku wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe mbalimbali.

“Maandamano yataanza saa 10:00 asubuhi katika eneo la bima, tutatembea hadi kituo kikuu cha mabasi, mnarani na kuelekea ofisi za klabu hiyo zilizopo jengo la Msalaba Mwekundu maeneo ya shangani mjini Mtwara” alisema samba na kuongeza

“Awali ilikuwa tufanye leo (Septemba,11, 2012) lakini polisi walituzuia kwa madai hawajajiandaa na kwa mujibu wa sheria tulitakiwa tuwataarifu saa 48 kabla”

Simba ametoa wito kwa watu wote wanaolaani mauaji hayo kuunga mkono waandishi wa habari kwa kushiriki katika maandamano hayo.

mwisho

Advertisements