WANAHABARI MTWARA WAANDAMANA

This slideshow requires JavaScript.

Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Mtwara leo (septemba, 12, 2012) wataandamana kimyakimya kupinga mauaji ya mwandishi wa habari mwenzao Daud Mwangosi aliyeuawa akiwa mikononi mwa polis

Mwangosi ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Iringa Press Club

Hassan Simba akisoma tamko

aliuawa kwa kulipuliwa na kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu.

Maandamano hayo yalioanza eneo la Bima yalivuta hisia za watu wengi waliojitokeza kandokando ya barabara huku waandishi wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe mbalimbali.

This slideshow requires JavaScript.

Maandamano hayo yalitia nanga ofisi za Klabu ya Waandishi wa Habari Mtwara ambapo mwenyekiti wake Hassan Simba alitoa tamko la kutoandiaka habari zenye mrengo chanya za jeshi la polisi ndani ya siku 40za maombelezo.

Mbalina hilo mwenyekiti huyo aliweka wazi kuwa kwa sasa wanahabari mkoani Mtwara wanaliangaliajeshi la polisi kama mdau mwenye mashaka, huku akitoa wito kwa wahusika kuchukuliwa hatua za kisheria mara moja.

maandamano

“Mauaji haya ni ya kinyama, udhalilishaji…mbaya zaidi yametokea mikononimwa polisi watu ambao tulidhani ndiyo usalama wa raia…tunasitisha utangazaji wa habari zenye mrengo chanya kwa jeshi la polisi kwa siku 40 tangu jana, kama ilivyokubaliwa najukwaa la wahariri” alisema Simba

Wanahabari hao walitembea umbali wa zidi ya kilomita Saba huku midomo yao ikiwa imefungwa kwa plasta ishara ya kuzuiwa kuongea hali iliyowavutia wengi

Mwisho