WANAHABARI MTWARA WANOLEWA HABARI ZA UCHUNGUZI

This slideshow requires JavaScript.

WANAHABARI wa mkoa wa Mtwara leo (Septemba, 17, 2012) wameanza mafunzo ya siku sita ya uandishi  wa habari za uchunguzi chini ya mkufunzi nguli wa habari za uchunguzi nchini, Fili Karashani.

Karashani ndiye mwandishi alitunukiwa tuzo ya mwandishi mwenye mchango uliotukuka kwa tasinia ya habari nchini kwa mwaka 2011. Moja ya mambo yaliyomng’arisha mwandishi huyo mkongwe ni kazi zake za habari za uchunguzi.

Mafunzo hayo yanaendelea mjini Mtwara yakijumisha wanahabari 18 kutoka vyombo mbalimbali yakiwa na lengo la kuwajengea uwezo kuandika habariz za uchokonozi.

Katibu Mkuu wa Klabu ya waandishi wa habari Mtwara, Abdallah Nassoro alisema mafunzo hayo yamefadhiliwa na Umoja wa Klabu za Waandishi nchini (UTPC).

Mwisho

Advertisements