NIMELALA KWA MIAKA 10, NISAIDIENI

This slideshow requires JavaScript.

Sofia Mashaka (37) mkazi wa kijiji cha Kilimanihewa wilayani Nanyumbu mkoani Mtwara kwa miaka kumi (10) sasa maisha yake yamekuwa kama mtoto mchanga anaetegemea mlezi wake kwa kila jambo.

Sofia tangu mwaka 2002 amekuwa ni mtu wa kulala, huku haja zote akijisaidia kitandani hapo baada ya kuanguka akiwa amebeba gogo kwa ajili ya kupasua kuni.

Kwa mujibu wa madaktari dada huyo ana matatizo ya uti wa mgongo kupata ufa, jambo ambalo linasababisha ashindwe kukaa, kusimama na hata kushika kitu mikononi mwake.

Jitihada za matibabu kwake zimekuwa ngumu baada ya kukosa fedha, hadi sasa hafahamu ni kiasi gani kinahitajika ili aweze kutibiwa.

“Natamani kufa kuliko kuendelea kuishi kwenye duania hii isiyo na msaada, imekuwa kama dunia ya wanyama wanaokimbiana pale mmoja anapopatwa na tatizo…sihitaji pesa bali nahitaji mtu anigharamie matibabu yangu, siwezi kusimama, kukaa, wala kula kwamikono yangu…ni heri ningekuwa kilema, lakini maumivu ya mgongo yanitesa sana” anasema Sofia

Kusini inawaomba Wasamalia wema kujitokeza kumsaidia dada huyu  ili kuokoa maisha yake na mateso anayoyapata .

Wasiliana na o787104785/0715104785.

Mungu awatangulie