CHILUMBA MWENYEKITI MPYA UVCCM MTWARA

This slideshow requires JavaScript.

UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (Uvccm) mkoa wa Mtwara, umemchangua Nestory Chilumba kuwa mwenyekiti wake mpya atakayeuongoza kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Chilumbaali aliwabwaga Slaji Mohamedi aliyepata kura 26 na Nasibu Haji aliyeambulia kura 171 kwa kupata kura 254 kati ya kura 478 zilizopigwa huku kura 27 zikiripotiwa kuharibika.

Msimamizi wa uchaguzi huo Alhaji Masoud Mbengule ambaye ni Katibu wa CCM mkoani  hapa alimtangaza Chilumba kuwa mwenyekiti mpya wa jumuiya  hiyo, katika mkutano mkuu wake wa uchaguzi uliofanyika jana ukumbi wa chuo kikuu cha Stella Maris mjini Mtwara.

Mara baada ya kutangazwa kuwa mwenyekiti chilumba alisema “Mshikano ndiyo kusudio letu, nashukuru sana kwa kuniamini nawaahidi kukiimarisha chama change, nipeni ushirikiano”

Alhaji Mbengule pia alimtangaza Mwidini Nannilah kuwa mjumbe wa baraza kuu la chama hicho taifa baada ya kushinda kwa kura 367 na kuwatupa wagombea watatu na kura zao katika mabano  Amani Mtepa (56) Rajabu Bakari (34) na Selemani Samkwa (6) kati kura 463 zilizopigwa.

Aidha nafasi ya ujumbe mkutano mkuu CCM Taifa ilitwaliwa na Amani Abdul kwa kura 277 katika kura za marudio na kumbwaga Muhidini Athumani aliyepata kura  130, huku Haji Hamisi akiondolewa katika duru ya kwanza ya uchaguzi huo baada ya kupata kura 107na kuzidiwa na wawili hao.

Msimamizi huyo  alimtangaza Palango Abdul kuwa Mjumbe mwakilishi jumuiya ya wazazi baada ya kupata kura 303 na kumpiku mpinzani wake aliyepata kura 39 katika kura za marudio, ambapo awali Bakari Mtumwene aliondolewa kwa kura 98.

“Nafasi ya Uwakilishi Jumuiya ya Waanawake (UWT) Taifa, wagombea walikuwa watatu, katika kura za awali Lilian Muhagaza alipata kura 128, Sauda Jafu kura 131 na Diya Mwanya kura 180, kwa kuwa hakuna aliyefikisha nusu ya wapiga kura 452, kura zilirudiwa kati ya Sauda na Diya…baada ya marudio Diya amepata kura 280 na Sauda 136…namtangaza Diya Mwanya kuwa mshindi wa nafasi hii” alisema Alhaji Mbengule

Mwisho

 

Advertisements