IBUENI MASUALA YALIYOJIFICHA KUHUSU GESI MTWARA

This slideshow requires JavaScript.

Waandishi wa Habari wa mkoa wa Mtwara wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuomba fedha kutoka Mfuko wa Habari Tanzania (TMF) ili waweze kuibua masuala yaliyojificha vijijini, yakiwemo ya gesi.

Wito huo umetolewa Oktoba, 9, 2012 katika ukumbi wa Bandari Klabu na Japhet Sanga ofisa wa programme na mafunzo wa mfuko huo.

Alisema mfuko huo unawezesha waandishi wa habari kwa kuwapa ruzuku hadi sh. 1.5 milioni kwa wazo la kihabari la uchunguzi hasa vijijini ili kupaza sauti za wanyonge.

“Fedha hizi ni kwa ajili ya waandishi wa habari, mapema Novemba mwaka huu tutatangaza kupokea maombi ya waandishi wa habari ya mawazo ya habari ya kiuchungzi” alisema Sanga

“Tunahitaji waandishi wa habari wa Mtwara waende kwa kina kuripoti habari za gesi na mafuta…tuache kuripoti mafuta yamegundulika…tuambieni kinachoendelea huku” alisisitiza

Akifafanua umuhimu wa uandishi wa habari za uchunguzi, mwandishi nguli, Ndemara Tangambwage alisema moja ya changamoto kubwa inayowakabili wanahabari nchini ni kukosa fedha za kwenda vijijini kuibua masula yenye maslahi ya umma yaliyojificha na kwamba kuwapo kwa mfuko huo ni mkombozi kwao.

Mwisho

Advertisements