WANAHABARI MTWARA WACHAMBUA SERA, BAJETI

This slideshow requires JavaScript.

WANAHABARI 18 wa mkoa wa Mtwara wananolewa juu ya uandishi wa habari unaozingatia uchambuzi wa sera na bajeti kwa siku nne.

Mfunzo hayo yaliyoanza Oktoba, 8, 2012 yatakamilika Oktoba 11 na kufanyika ukumbi wa Klabu ya waandishi wa Habari mkoani Mtwara.

Mwenyekiti wa Klabu hiyo Hassan Simba, mafunzo hayo yamefadhiliwa na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) na yanawezeshwa na mtaalam wa habari na uchambuzi wa sera na bajeti, Adam Ndokeji kutoka jijini  Mwanza.

“Ni muendelezo wa mafunzo yanayolenga kuwanoa wanahabari Mtwara ili kuimarisha taaluma yao…mafunzo haya yamefadhiliwa na UTPC…waandishi 18 wanashiriki” anasema Simba

Akiwezeshamafunzo hayo, Ndokeji anasema iwapo wanahabari watatambua umuhimu wa kuchambua sera katika habari zao, licha ya kuongeza ubora wa kazi zao pia itaongeza heshima za kazi zao.

Mwisho

Advertisements