Mkuchika, Ghasia wambwaga Murji, Walisakata ruba ukumbini.

This slideshow requires JavaScript.

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora, Goerge Mkuchika na Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serekali za Mitaa ( Tamisemi), Hawa Ghasia jana walijikuta wakiongoza mamia ya wana CCM wenzao kusakata rumba baada ya kushindwa kuzuia furaha zao zilizosababishwa na ushindi wa mgombea waliokuwa wakimuunga mkono katika nafasi ya uwenyekiti wa chama hicho mkoani hapa.

Mkuchika na Ghasia muda wote baada ya kutangazwa kwa matokeo yaliyompa ushindi Mohamedi Sinani walikuwa wakiinua mikono juu kusakata rumba huku vicheko na tabasamu vikitawala midomoni mwao hali iliyohamasisha wafuasi wao kuzidisha shangwe ukumbini humo.

Uchaguzi huo uliofanyika ukumbi wa shuleya sekondari ufundi mjini Mtwara, uliwaweka wagombea na wafuasi wao roho juu hadi saa 2 usiku ambapo msimamizi mkuu wa uchaguzi huo Sophia Simba alipoingia ukumbini kutangaza matokeo.

Akitangaza matokeo hayo Simba ambaye ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM Taifa , alisema Sinani ambaye alikuwa mbunge wa Mtwara Mjini 2005/10 alimshinda Jamadin Mtonya baada ya kupata kura 533 kwa 462 kati ya 1003 zilizopigwa huku kura nane zikiripotiwa kuharibika.

Alisema kwa matokeo hayo Sinani ndiye mwenyekiti mpya wa CCM mkoa wa Mtwara, na kwamba uchaguzi ulifuata taratibu zote za kisheria na kanuani za chamahicho

Ushindi wa Sinani ulipatikana katika kura za marudio baada ya awamu ya kwanza wagombea wote kushindwa kufikia nusu ya kuza zote 1003 zilizopigwa.

“Matokeo ya awali yalikuwa, Victor Mmavele alipata kura 49, Mtonya kura 459 na Sinani kura 495, hakuna aliyefikia nusu kwa hivyo ndiyo maana tuliamua kurudia kwa wagombea wawili waliopta kura nyingi na sasa haya ndiyo matokeo yake”

Uchaguzi huo ulivuta hisia za watu wengi kufuatia makundi makubwa mawili yaliyokuwa yanakinzana ambapo kundi jinyine liliongozwa na Mbunge wa Mtwara Mjini Asnain Murji na Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa (Nec) CCM wilaya ya Mtwara mjini Godbleee Kweka lililojipa nafasi kubwa ya kutwaa ushindi.

“Siko kwenye ‘mood’ (hali) mzuri ya kuzungumzia hilo, labda munitafute baadae” alisema Mtonya alipotakiwa kuzungumzia namna ambavyo alivyoyapokea matokeo hayo.

Kwa upande wake Sinani aliwashukuru wana CCM mkoani hapa kwa kuonesha kuwa na imani nay eye na kuahidi kukiimarisha chama huku akisisitiza mshikamano ndiyo silaha kuu.

“Nashukuru kwa kuonesha imani na mimi…nitaimarisha chama chetu, kubwa niombe ushirikiano kutoka kwenu wanachama” alisema Sinani.

Aidha Simba  aliwatangaza washindi wa nafasi ya ujumbe wa halmashauri kuu  ya mkoa kutoka wilaya ya Mtwara Vijijini kuwa ni Fatuma Makopo (320), na Zainabu Namkwanga (390), wilaya ya Tandahimba Jamadini Mtonya (293) na Salma Abdallah (304), wilaya ya Masasi Charles Chikomele (440) na Blandina Nakajumo (562).

Msimamizi huyo alitangaza kuwa katika wilaya ya Mtwara Mjini, Salma Chitope (349) na Hawa Mangasala (353), wilaya ya Nanyumbu, Hawa Akwiti (350) Rajab Mrope (447) na wilaya ya Newala Lidia Boma (384) na Hamis Nakuya (510)

Mwisho

Advertisements