MFUKO WA JIMBO WANUFAISHA WAJASILIAMALI TANDAHIMBA

Juma Njwayo

VIKUNDI Sita vya wajasiliamali wa wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara vimenufaika na mfuko wa jimbo kwa kuwezeshwa fedha tasilimu sh. 1 milioni kwa kila kimoja ili kuinua mitaji yao.

Akikabidhi fedha hizo jana mbunge wa jimbo hilo, Juma Njwayo alisema ofisi yake imeamua kuviwezesha vikundi hivyo ikiwa ni hatua mojawapo ya kutekeleza makakati wa kuwawezesha vijana kiuchumi ili kukabilina na hali duni ya maisha inayowakabili.

Alisema vikundi hivyo Sita ni miongoni mwa vikundi Tisa, vilivyoomba kuwezeshwa na mbunge huyo na kwamba vikundi vitatu vilivyobakia vitasaidia kiasi kama hicho hivi karibuni.

“Vijana hawa hawajakaa kijiweni na kuomba kuwezeshwa, kwanza wameonesha nia ya kujikwamua na matatizo waliyonayo na ndipo walipoomba msaada, nimeamua kuwasaidia …. Naomba niweke wazi kuwa fedha hizi zinatoka mfuko wa jimbo ambao mimi mbunge wenu nausimamia” alisema Njwayo katika makabidhiano hayo

Alifafanua kuwa “Ni vigumu kwangu iwe kwa fedha zangu binafsi au za mfumo wa jimbo kumwezesha mtu mmoja mmoja lakini pale munapojiunga katika vikundi kama hivi kwangu ni rahisi kuwasaidia”

Vikundi vilivyonufaika na fedha hizo ni Lawi dev, Abujahari , Nuruwaiti na Vijana vinavyojishughulisha na uselemala, kikundi cha Umoja kinajishuhulisha na ubanguaji wa korosho na kingine ni cha vijana wanaotoa huduma za usafiri wa pikipiki, vyote vya mjini Tandahimba.

Akizungumza kwa naiaba ya vikundi vingine Katibu wa Kikundi cha Vijana workshop Bashiri Nanguo alimshukuru mbunge huyo kwa kuwawezesha wajasiliamali wadogo kukuza mitaji yao.

“Nashukuru kwa msaada tuliopewa, sisi wajasilimali wadogo kilio chetu hasa ni ukosefu wa mitaji, kwa hizi fedha tulizopewa zitasaidia kuinua biasharasha zetu na hali ya maisha…tunaomba aiishie hapa, hata kwa kutumia fedha zake mwenyewe aendelee kuwawezesha wajasilimali wadogo wa jimboni kwake” alisema Nanguo

Aliongeza kuwa “kwanza ametuweka wazi kuwa ni fedha za mfuko wa jimbo, wengine wasingesema hivyo, pia angemua angetumia kwa mambo mengine lakini yeye aliona bora atusaidie sisi wajasiliamali wadogo sina budi kumpongeza”

Mwisho

Advertisements