BANDARI MTWARA KORTINI KWA KUPORA ENEO

This slideshow requires JavaScript.

WAKAZI wa Kitongoji cha Ng’wale kijiji cha Sinde Kata ya Msangamkuu, halmshauri ya Mtwara kesho wanatarajia kuifikisha Mahakama Kuu Mamlaka ya Bandari mkoani hapa kwa madi ya kutwaa eneo lao kinyume cha sheria.

Akizungumza na KUSINI juu ya kusudio hilo leomjini Mtwara mweyekiti wa kamati teule ya kufuatilia suala hilo Marijani Dadi alisema wamefikia uwamzi huo baada ya jitihada za kumaliza mgogoro huo kwa njia ya mazungumzo kutozaa matunda.

Alifafanua kuwa mwaka 2000 mamlaka hiyo bila ya kushirikisha kijiji walitwaa eneo la kitongoji cha Ng’wale kwa ajili ya upanuzi wa bandari bila ya kushirikisha uongozi wa serikali na wamiliki wa asili wa maeneo hayo.

“Tugeweza kusema tunadai fidia iwapo utaratibu wa kutwaa eneo husika ungekuwa umefuatwa…si uongozi wa kijiji wala wamiliki wa asili wa maeneo hayo walioshirikishwa katika utwaaji wa neo hilo…sisi tunaona tunadhulumiwa haki yetu” alisema Marijani

Aliongeza kuwa “Takribani wakazi 300 wa kitongoji cha Ng’wale ndiyo tunaolalamikia kudhulumiwa kwa haki yetu…kesi tumefungua Mahakama Kuu kitengo cha ardhi…ni kesi ya madai na kwa upande wetu itasimamiwa wakili maarufu nchini Dk. Ringo Tenga”

Mwenyekiti huyo wa kamati ya hiyo teule iliyoundwa na wanakiji hao alisema kuwa walifikisha suala hilo wizara ya ardhi nyumba na makazi kwa utatuzi bila mafanikio na kwamba tegemeo lako katika kupata haki yao kwa sasa ni Mahakama.

Mwisho.

Advertisements