TAMASHA LA NGOMA ZA ASILI KUTIKISA MTWARA

Mkurugenzi Mwenza wa ADEA, Philipo Lulale (Katikati) akizungumza na waandishi wahabarii mjini Mtwara

TAMASHA la ngoma za asili la makabila ya Wamakonde, Wamakuwa na Wayao linalojulikana kama MaKuYa linatarajia kutikisa mkoa wa Mtwara Novemba, 17, 81 mwaka huu.

Tamasha hilo litakalodumukwa siku mbili mfululizo litashirikisha jumla ya vikundi 20 vya ngoma za asili kutoka wilaya zote tano za mkoa wa Mtwara zikiwa namchanganyiko wa makabila hayo, litashindikizwa na michezo ya asili na maonesho ya bidhaa za asili.

Mkurugenzi Mwenza wa Kituo cha Maendeleo ya Utamaduni na Sanaa za Afrika (Adea) Philipo Lulale amesema tamasha hilo la nne kuandaliwa na kituo hicho tangu mwaka 2008, ambapo kwa mwaka huu litashirikisha jumla ya wasanii 400.

“MaKuYa itawaweka pamoja wasanii hao wapigaji na wachezaji wangoma za asili kutoka katika wilaya za mkoa wa Mtwara kwa upande mmoja na maonesho ya bidhaa za asili na michezo ya jadi kwaupande mwingine” alisema Lulale

Alifafanua kuwa “Kwa lengo la kuhifadhi utamaduni huo kabla hatujachelewa , tamasha la MaKuYa litakutanisha tena wasanii wacheza ngoma zaidi ya 400 katika vikundi 20 kutoka makabila makubwa matatu ya mkoa wa Mtwara”

Alisema madhumuni ya tamasha hilo ni kuwa jukwaa la kila mwaka kwa ajili ya wasanii wa mkoa wa Mtwara kupiga na kucheza ngoma za asili, kudhibiti na kuhimiza utamaduni wa asili na kukuza mapenzi ya utamaduni wa mkoa wa Mtwara.

Mkurugenzi mwenza huyo alisema tamasha hilo lililofadhiliwa na ubalozi wa Finland, British Gas (T) Ltd, Wentworth Foundation na ODJILL DRILLING litatoa fursa ya wazawa na wageni zaidi ya 1300 hadi 1500 kutembelea viwanja vya Nangwanda Sijaona mjini Mtwara ambako litafanyika.

Ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi ili waweze kuona sanaa za asili ambazo ndiyo urithi uliohamishika.

Mwisho