UMRI WA KUGOMBEA URAIS, UBUNGE UONGEZWE

This slideshow requires JavaScript.

MKAZI wa kijiji cha Msijute, Halmashauri ya Mtwara, mkoani hapa Mahamudu Kambona (48) ametaka muda wa Mtanzania kuruhusiwa kugombea urais na ubunge uongezwe badala ya umri wa sasa.

Akitoa maoni yake mbele ya Tume ya kukusanya maoni ya Katiba, kijijini hapo leo Kambona alisema umri wa mtu kugombea urais unapaswa kuongezwa kufikia miaka 45 kutoka 40 ya sasa.

Alisema ongezeko hilo pia linahusu umri wa mtu kugombea ubunge, ambapo alipendekeza umri huo uwe miaka 25 badala ya 21 ya sasa.

“Naomba mda wa mtu kugombea urais uongezwe na kufikia 45 badala ya 40 ya sasa na ubunge iwe miaka 25 badala ya 12” alisema Kambona

Aidha mwanakijiji huo alipendekeza pia kuwapo kwa Makamu wawili wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Watanzania.

“Iwapo Rais atatoka Zanzibar, makamu wa kwanza wa rais atoke Tanzania bara na makamu wa pili atatoka Zanzibar…Iwapo Rais atatoka Tanzania bara basi Rais wa Zanzibar awe Makamu wa Kwanza wa Rais” alisema mwanakijiji huyo.

Pia Kambona alipendekeza kufutwa kwa adhabu ya kifo kwa kuwainakiuka haki ya msingi ya binadamu ya kuishi.

Katika mkutano huo ulioendehswa na mwenyekiti Sengondo Mvungi, ulitanguliwa na maelezo ya umuhimu wa kutoa maoni ya Katiba yaliyotolewa na mjumbe wa Tume hiyo, Kibibi Hassan ambaye aliwaambia ni wakati muafaka kwao kutengeneza katiba waitakayo.

“Tumieni fursa hii kutoa maoni yetu…jisikieni huru, utakachosema ndicho kitakachonukuliwa, baada ya hapa tutarudi kwenu tukiwa na rasim ya Katiba, safari hiyo tutaiwasilisha kwenu kupitia mabaraza ya wilaya” alisema Hassan

Aliongeza kuwa “Tutaipeleka kwenye Bunge maalum la Katiba na baada ya hapo italewata kwenu kwa ajili ya kupigia kura ya ndiyo na hapana…msiwe na wasiwasi, hii ni Katiba yenu”

Mwisho

 

 

Advertisements