GHASIA ‘AWAKA’ UCHELEWESHAJI UJENZI BARABARA MTWARA

This slideshow requires JavaScript.

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Hawa Ghasia ameelezea kukerwa kwake na maendeleo duni ya mradi wa ujenzi wa barabara za mji wa Mtwara unaotekelezwa chini ya mradi wa benki ya Dunia wa uendelezaji wa Majiji.

Akizungumza jana mara baada ya kukagua mradi huo, Ghasia alionesha wazi kukerwa na kitendo cha Mhandisi Msahauri Mkazi kutopatikana eneo la kazi na hajulikani halipo, ambapo aliagiza mamlaka zake kumwajibisha kwa kushindwa kusimamia vema mradi huo.

Tayari awamu mbili za utekelezaji wa mradi huo zimefikiwa ambapo awamu ya kwanza ujenzi wa barabara za Zambia yenye urefu wa kilomita 3.77 na Bandari yenye urefu wa kilomita 2.75 zinajengwa upya kwa kiwango cha lami na kuwekwa taa za barabarani wakati kilomita 1.9 itajengwa kwa kiwango cha tofali za saruji katika mji mkongwe wa Mikindani.

Taarifa zinasema kuwa mradi huo wa awamu ya kwanza unatatekelezwa na kampuni ya kandarasi ya Southern Link ambayo kwa mujibu wa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo ilipaswa kufikia asilimia 80 ya utekelezaji, hata hivyo hadi sasa imefikia asilimia 40 tu ikiwa imebakia miezi mitatu kwisha kwa mda wa mkataba, mradi ambao umegharimu 12.7 bilioni.

Awamu ya pili ya ujenzi wa barabara ya Kunambi yenye urefu wa kilomita 1.8 na ya Chuno yenye urefu wa kilomita 5.88 unaotekelezwa na kampuni ya Shaprya ambayo ilipaswa hadi sasa iwe imefikia asilimia 35 ya utekelezaji na imefikia asilimia 22.

“Natoa wiki mbili kwa manispaa, mkoa na Tamisemi mchukulieni hatua mshauri mkazi wa mradi huu…maana ya kuitwa mkazi inabidi akae hapa kusimamia maslahi ya serikali na Taifa, mradi huu haufanyi vizuri kwa sababu yeye hayupo” alisema Ghasia

Aliongeza kuwa “Wala siwatishi, fanyeni mchezo …siko tayari kuvuna mabua maana ukicheka na nyani utavuna mabua…sina time (mda) wa kulea wabovu…sitaki hadithi katika hili”

Waziri huyo alisema kuwa hajaridhishwa na kasi ya ujenzi kitendo ambacho alisema hatakubali kuona kikiendelea ili hali wahuska hawajawajibishwa.

“Ni manispaa mbili tu ndizo zimetoa zabuni kwa kampuni za wazawa, Mtwara na Kigoma, hizo zote hazifanyi vizuri katika huu mradi…wenzetu wazawa mnatuangusha, fanyeni kazi tudhihirishe kuwa wazawa tunaweza” alisema Ghasia

Kwa upande wake Naibu Meya wa Manispaa hiyo, Zalali Zalali alisema ucheleweshwaji wa uondoaji wamiundombinu ya maji, simu na umeme umechagiza kudhorota kwa ujenzi huo.

“Hata sisi madiwani tulibaini kasi ya ujenzi wa mradi huu wa kwanza unaotekelezwa na Southern Link hauwendi vizuri…kule Mikindani mgefika ndiyo hakujaguswa kabisa” alisema Zalali

mwisho