SERIKALI:HOJA YA WANA-MTWARA TUMEISIKIA

This slideshow requires JavaScript.

SERIKALI imesema imeyapokea malalamiko ya wananchi wa Mtwara ya kupinga kusafirishwa gesi asilia inayochimbwa mkoani humo kwenda Dar es Salaam kwa njia ya bomba.

Makamu wa Rais Dk. Mohamedi Ghalib Bilal aliyasema hayo jana katika ukumbi wa Veta mjini hapa alipokuwa anazindua mradi wa kukuza ajira kupitia vyuo vya ufundi stadi unaotekelezwa chuo hicho kwa ushirikiano wa Britishi Gas (BG) Tanzania, na VSO ya Uingireza.

“Nimekusikieni wana-Mtwara malalamiko yetu, munahoji kwanini gesi iende Dar es Salaam…manufaa ni mengi yanakuja kwa wakaziwa Mtwara, Mtwara ina nafasi kubwa, kuna watu wengi wanaomba kuwkeza” alisema Bilal

“Lazima tufanye kazi kwa pamoja kujenga misingi ya kuhakikisha wote tunafaidika na gesi…tujipange kufaidika”aliongeza Dk. Bilal huku akikwepa kuzungumziakwa kina suala hilo

Dk. Bilal alibainisha kuwa mradi huo wa miaka mitatu kuanzia mwaka huu, unalenga kuwanufaisha wanafunzi 280 ambao watakuwa wamehitimu kwa ngazi ya kimataifa na kuwawezesha kupata ajira Duniani kote.

“Natoa ombi kuwa makampuni mengi yajitokeze kushiriki karika mradi huu kwani una mafanikio makubwa si kwa wahitimu peke yake bali kwa makampuni pia kwani watapata wafanyabishara mahiri watakao tumia mda mfupi kuelewa wajibu wao…nawashukuru washiriki wote wa mradi” alisema Dk. Bilal

Awali Mkurugenzi wa Mafunzo wa Veta Nchini, Leah Lukindo alisema mradi huo unalenga kuwajengea uwezo wahitimu kupata ajira katika makampuni ya uchimbaji na utafiti wa gesi na mafuta ndani na nje ya nchi na hivyo kupunguza tatizo la ajira.

“Wahitimu wataweza kuajiriwakwenye makampuni ya gesi na mafuta duniani kote kwa sababu vyeti watakavyopata vitakuwa na viwango vya kimataifa…watapata mishahara mizuri na hivyo kuboresha maisha yao”

Alisisitiza kuwa “Mwanafunzi 280 wamegawanyika katika kozi za kuchomea, bomba, uselemala, mapishi, na kujifunza lugha ya kiingereza katika viwango vya kimaiatafa”

Kwa upande wake Meneja waBritish Gas ( BG) Tanzania, Matt Wilksalisema mafunzo hayo ya miaka mitatu yatagharimu dola za kimarekani 1milioni.

Kabla ya ufunguzi wa mafunzo hayo Makamu wa Rais alifungua jengo la ofisi ya Veta kanda ya kusini mashariki, ambapo  Mkurugenzi wa veta nchini, Mhandisi Zebadiah Moshi alisema ofisi hiyo itahusika na uandaaji wa mitaala ya Veta kulingana na mahitaji ya soko.

“Ofisi hii itahusika pia na utafiti wa soko la ajira kwa vijana na kuandaa mitaala itakayokidhi mahitaji hayo” alisema Moshi.

Mwisho

Advertisements