MTWARA KUPANDISHA BENDERA YAO

Mwenykiti wa UDP Mtwara mjini Seleman Chimpele akihutubia mkutano

Mwenykiti wa UDP Mtwara mjini Seleman Chimpele akihutubia mkutano

VYAMA Sita vya  siasa vya upinzani vya wilaya ya Mtwara vimeungana kuendesha mikutano ya adhara ya kuhamasisha wananchi wa mkoa huo kupinga gesi asilia kupelekwa Dar es Salaam kwa njia ya bomba.

Katika kutengeneza umoja huo vyamahivyo vimekubalina kutengeneza bendera ya Mtwara itakayopandishwa kuashiria umoja wa wananchi hao katika kutetea rasilimali yao.

Tayari Rais Jakaya Kikwete amezindua mradi wa ujenzi wa bomba hiyo huko Kinyelezi jijini Dar es Salaam mwezi mmoja uliopita, kitendo kinachopingwa na wakazi wa mikoa ya kusini hususani Lindi na Mtwara.

Hoja za wananchi za kupinga gesi kwenda Dar es Salaam zilisababisha kuzomewa kwa mawaziri watatu mbele ya katibu mkuu wa CCM, Abdulahman Kinana alipofanya mkutano wa adhara soko kuu  mjini Mtwara hivi karibuni.

Jana viongozi wa vyama vya siasa  Sita, NCCR Mageuzi, APPT Maendeleo, TLP, ADC, Chadema  na UDP walianza mikutano ya kupinga kuhamishwa kwa gesi katika viwanja vya Mkanaledi.

Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, Uledi Hassan Abdallah alisema wapo tayari kupinga gesi kupelekwa Dar es Salaam kwa njia ya nguvu ya umma na mahakama.

“kwa hali ilivyo ni njia mbili tu zinaweza kuokoa gesi yetu isipelekwe Dar es Salaam, moja kwa njia ya maandamano, pili mahakama” alisema Uledi

Alifafanua kuwa “Gesi ikihamishwa mikoa ya kusini itaendelea kuwa masikini hadi mwisho wa dunia…tuseme inatosha, tuwe tayari kutetea maslahi yetu kwa ajili ya vizazi vyetu”

Alisema katika awamu hiyo ya kwanza mikutano minne itafanyika ikitanguliwa na kauli mbiu “Gesi kwanza, vyama baadae, hapa hakitoki kitu”

Katibu wa TLP wilaya ya Mtwara, Hayadhi Walilanga alisema ili kufanikisha hilo bendera moja itatengenezwa ambayo itajulikana kama bendera ya Mtwara ambayo itakuwa kama ishara ya muungano wao katika kueteta gesi.

“Wachoraji watuandalie bendera moja itakayotambulisha Mtwara katika kutetea rasilimali yao ya gesi isiporwe na wachache….tutaipandisha kila kwenye mkutano wetu” alisema Walilanga.

Mwisho