WAANDISHI MTWARA WANYOSHEWA KIDOLE ISHU YA GESI

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mtwara, Hassan Simba

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mtwara, Hassan Simba akihojiwa na waandishi wa habari wa mkoa huo

WAANDISHI wa Habari mkoani Mtwara wametupiwa lawama na Muungano wa vyama vya siasa vya upinzani vinavyopinga gesi asilia inayochimbwa mkoani humo kupelekwa Dar es Salaam kwa kutoripoti bahari hizo kwenye vyombo vyao.

Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, Uledi Abdallah alisema jana katika mkutano wa adhara uliofanyika eneo la Soko kuu kuwa “Tunamashaka na hawa waandishi wetu wa habari, tangu tumeanza mikutano yetuhatujasikia kwenye magazeti wala TV”

Alishtumu kuwa kutkana na ukimya huo muungano huo unahisi waandishi wa hbari mkoani humo ‘wamefungwa mdomo’ na serikali ili wasitangaze.

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Mtwara, Hassan Simba amepinga madai hayo ya wanasiasa na kuongeza kuwa vyombo vya habari mkoani humo vipo huru kuripoti habari yeyote.

“Huku wakizingatia maadili ya taaluma yao, waandishi mkoani kwangu wapo uru, huru kabisa kuripoti habari zozote zile kwa ngazi yeyote, iwe gesi au jambo lingine…hakuna uhusiano wa waandishi kutoandika habari hizo na kufungwa mdomo” alisema Simba

Aliongeza kuwa “Tatizo watu hawajui kuwa waandishi sio ‘final say’ ya kuruhusu habari ichapishwe…nitafuatilia kuona ni katika mazingira gani habari hizo hazitoki katika vymbo hususani vya kitaifa”

Hivi karibuni vyama vya upinzani vya siasa vimefunga ndoa ya kutetea gesi isinde Dar es Salaam kwa madai kuruhusu hivyo ni kuiangamiza mtwara ambayo ipo nyuma kimaendeleo.

Mwisho

Advertisements