MKAPA AKWEPA KUZUNGUMZIA GESI

Benjamin Mkapa

Benjamin Mkapa

RAIS Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa amemaliza kuhutubia wananchi katika Zahanati ya Imekuwa Mtwara vijijini huku akikwepa kugusia suala la gesi.

Mkapa alifika kijijini hapo kwa ajili ya kukabidhi nyumba 30 za madaktari zilizojengwa na Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation.

Hali hiyo ni kinyume na matarajio ya wakazi wengi wa mikoa ya kusini ambao waliamini angeweza kugusia sula la gesi japo kwaujumla wake.

Mkapa ambaye alionekanakuchagua manenoya kuzungumza alionesha kujikita zaidi kweye kuwataka madaktari kujenga moyo wa kizalendo wa kufanya kazi maeneo ya vijijini.

“Mkihamishiwahuku msikimbie, fanyeni kazi kwani Serikali inawaandalia mazingira mazuri ya kufanyakazi…huku vijijini wanaishi watuna wanataka huduma zanu” alisema Mkapa huku akishangiliwa.

Baadhi ya wananchi walioudhuria hafla hiyo walionesha kushangazwa kwake na kitendo cha Mkapa kukwepa kuzungumzia suala nyeti la gesi ambalo ajenda kwa wakazi wa mikoa ya kusini.

“Labda ameambiwa asizunguzie hilo na viongozi wengine” alisema Jabir Ally

MWisho