MKAPA KUZUNGUMZIA GESI LEO?

Benjamin Mkapa

Benjamin Mkapa

RAIS Mstaafu wa awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa leo anatarajia ‘kunguruma’ katika hafla fupi ya kukabidhi nyumba 30 za madaktari zilizojengwa na taasisi ya Mkapa Foundation.

Katika Zahanati ya Imekuwa wilaya ya Mtwara mkoani Mtwara Mkapa anatarajia kuzungumza na wananchi na Taifa kwa ujumla kuhusu masuala ya afyana mambo mengineyo.

Swali la msingi ambalo watu wa Mtwara wamekuwa wakijiuliza ni iwapo katika hotuba yake atazungumzia suala la gesi kupelekwa Dar es Salaam ukinzingatia yeye ni mzawa wa mkoa wa Mtwara.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na taasisi hiyo kwa vyombo vya habari Mkapa ambaye ni mzaliwa wa kijiji cha Mtojo-Lupaso, wilayani Masasi atakabidhi nyumba 30 kwa halmashauri ya Mtwara, Masasi na Newala ikiwa nyumba 10 kila moja.

Baadhi ya wananchi wamekuwa na shauku kubwa ya kusikiliza hotuba yake wakiamini inaweza kugusia sula nyeti lakupinga  gesi kwenda Dar es Salaam ambalo kwa sasa limekuwa ajenda ya moto kwa wakazi wa mikoa ya kusini.

Taarifa hiyo haijasema nini Mkapa atazungumzia katika hotuba yake, hata hivyo wengi wamekuwawakihitaji mawazo yake juu ya suala la gesi kwa madi kuwa kauli hiyo inaweza kutoa mwangakwa wananchi hao.

“Mkapa ni mwana kusini mwezetu, ningefurahi sana iwapo angezungumzia msimamo wake juu ya gesi…yeye anasemaje, iende Dar es Salaam isiende?” alihoji Abdallah Saed mkazi wa Mtwara.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo nyumba kupitia mradi huo nyumba 90 zimejengwa katika mikoa ya Mtwara, Katavi na Rukwa ambapo kila mmoja umepata nyumba 30.

Mradi huo unaofadhiliwa na shirikika la kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu Duniani umewezesha madaktari kuwa na makazi karibu na nyumba zao na hivyo kuboresha ufanisi wa kazi.

Mwisho

Advertisements