wAANDISHI WASOTA SAA 2 KUONANA NA MADAKTARI MTWARA

Waandishi wa Habari mkoani Mtwara wakisubiri kuongea na wataalam wa afya hospitali ya mkoa Ligula, leo

Waandishi wa Habari mkoani Mtwara wakisubiri kuongea na wataalam wa afya hospitali ya mkoa Ligula, leo

WAANDISHI wa Habari 18 walio katika mafunzo ya uandishi wa habari za afya leo (Desemba, 20, 2012) walisota kwa mda wa saa mbili kutoka saa tatu asubuhi hadi saa sita wakisubiri kuonana na uongozi wa hospitali hiyo kupata taarifa mbalimbali za afya.

Kundi hilo la waandishi lilisababisha wagonjwa kuduwaa, huku wahusika wakionesha kukwepa kuzungumza nao hali liyosababisha malalamiko kutoka kwa waandishi hao.

Waandishi hao mara kadhaa walisikika walilalama kuwa wamekaa kwa mda mrefu bila ya kufanikisha adhima yao, huku wengine walilalama ‘njaa’

“Njaa inauma, hapa nilipo hali tete” alisikika mmoja wa waandishi hao.

Hata hivyo ilipofika saa sita mchana madaktari na wataalam hao waliridhia kuongea na waandishi wa habari hao.

3

Advertisements