MAELFU WAANDAMANA MTWARA KUPINGA GESI KWENDA DAR

Waandamanaji Mtwara- gesi haitoki

Waandamanaji Mtwara- gesi haitoki

MAELFU ya Wakazi wa mkoa wa Mtwara leo wameandamana kutoka kijiji cha Mtawanya umbali wa kilomita Tisa kutoka Mtwara mjini barabara ya kwenda Msimbati eneo ambalo gesi asilia inavunwa hadi viwanja vya mashujaaa wakipinga uwamuzi wa serikali wa kusafirishwa gesi kwa njia ya bombakutoka mkoani humo kwenda Dar es Salaam.

Maandamano hayo ambayo yaliudhuriwa na wananchi kutoka baadhi ya wilaya ya mkoa wa Mtwara, zikiwemo Tandahimba na Newala yamefanyika kwa hali ya amani na utulivu huku yakisindikizwa na ulinzi mkali wa polisi.2

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na waratibu wa maandamano hayo, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Joseph Simbakali alipaswa kuwa mgeni rasmi hata hivyo alikataa na badala yake yalipokelewa na mwenyekiti wa umoja wa vyama vya siasa Hussen Mussa Amiri.

Vyama vilivyounda umoja huo ni Chadema, NCCR-Mageuzi, SAU, TLP, APPT Maendeleo, ADC, VDP na DP, vikiwa na kaulimbiu ya gesi kwanza vyama baadeye, hapa hakitoki kitu.

Soko kuu la mjini hapa, lilifungwa kwa mda hadi maandamano hayo yalipotia nanga, kutoa fursa kwa wafanyabiashara hao kushiriki katika maandamano hayo ambayo yalisababisha barabara kufungwa kwa mda.

Mabango yalitumika zaidi kuwasilisha ujumbe wa wananchi hao wa kupinga gesi kupelekwa Dar es Salaam ambapo baadhi yalisomeka “Bandari Bangamoyo, Viwanda Bagamoyo, Gesi Bagamonyo, Mtwara wapuuzi?….Gesi haitoki hata kama hatujasoma……gesi kwanza vyama baadae, hapa hakitoki kitu….kusini tumezarauliwa vya kutosha sasa baasi” yalisomeka baadhi ya mabango.

Akisoma tamko la vyama vya siasa vya upinzani vilivyoungana kupinga gesi kwenda Dar es Salaam katibu wa umoja huo, Seleman Litope kwa mda mrefu kusini imekuwa zikiondolewa fursa mbalimbali za maendleo, akitolea mfano wa kung’olewa kwa reli, ukosefu wa usimamizi mzuri wa zao la korosho, ukosefu wa miundombinu ya barabara, kuodnolewa kwa mradi wa maendeleo ya ukanada wa Mtwara (Mtwara coridor ) na kuondolewa kwa gesi.3

Alisema hali hiyo imesababisha mikoa ya kusini kuwa nyuma kimaendeleo na kwamba hawako tayari kuona historia ikijirudia na kwamba umoja wao wa vyama Nane vya siasa unalenga kuhakikisha rasilimali yao hiyo haitoki kwenda kokote kabla ya kuwanufaisha.

“Ujenzi usitishwe…serikali hadi leo haiko wazi namna gani wakazi wa Mtwara watanufaika na gesi hiyo wakati rais ameshazindua ujenzi wa bomba kwenda Dar es Salaam…uwamzi wa kupeleka gesi Dar es Salaam unapingana na tamko la Rais Jakaya Kikwete alilolitoa kwenye ziara yake mkoani Mtwara 2009 kwamba mkoa wa Mtwara ujiandae kuwa ukanda wa viwanda” alisema Litope

Taarifa hiyo imebainisha kuwa “Tuna hofu kutokana na ilivyokuwepo kwa wakazi wa Songongo (Lindi) kubaki masikini wakati gesi inazalishwa hapo, yasije yakatukuta sisi hivyo ni lazima tusimamie rasilimali hii ili iweze kuleta maendeleo”

Tamko hilo lenye kurasa mbili likiwa na maadhimio tisa linahoji kwanini mitambo ya kuzalisha umeme isijengwe Mtwar wakati eneo kwa ajili ya ujenzi huo linapatikana.

Aidha waandamanaji hao wamemuomba Rais Kikwete kumuondoa madarakani Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Joseph Simbakalia kwa madai amewatusi wananchi wa mkoa huo kwa kuwaita wapuuzi kutokana na madai yao ya kupinga gesi kwenda Dar es Salaam.4

“Tunamuomba Rasi Jakaya Mrisho Kikwete amuondoe katika nafasi ya ukuu wa mkoa  ndugu Joseph sombakalia na kutuletea mwingine kwa sababu ametutukana hadharani, tumeshindwa kuvumilia, HATUMTAKI” ilisema sehemu ya tamko hilo.

Mwisho

Advertisements