GESI ‘YAMCHEFUA’ MKAPA

Benjamin Mkapa

Benjamin Mkapa

DESEMBA, 27 mwaka huu ni siku ya kihistoria kwa wakazi wa mkoa wa Mtwara, ni siku ambayo waliandamana kupinga gesi asilia inayovunwa mkoani humo kupelekwa Dar es Salaam kwa njia ya bomba.

Katika maandamano hayo si mbunge wala kiongozi wa serikali aliyekuja rasmi kushiriki ama kuwasikiliza licha ya kwamba mkuu wa mkoa huo, Joseph Simbakalia ndiye aliyealikwa kuwa mgeni rasmi, hata hivyo alikacha na kuwaita wapuuzi waandamanaji hao.

Uchunguzi uliofanywa na KUSINI umebaini kuwa siku ya maandamano hayo wabunge, wakuu wa wilaya, mkuu wa mkoa na viongozi wa CCM walikuwa wilayani Masasi mkoani hapa wakiteta na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa.

Ni katika nyumba yake iliyoko mtaa wa Misufini, upande wa kushoto kama unaelekea Newala ndipo kikao hicho ambacho naweza kukiita “kitchen part” kwa viongozi wa mkoa wa Mtwara likipofanyika.

Vyanzo vyetu vya habari cinadokeza kuwa ulizni uliimarishwa siku hiyo ili kuzuia watu ambao sio waalikwa kusogelea eneo hilo.

Waandishi wa Habari wa Channel Ten mkoani hapa John Kasembe ni miongoni mwa waliozuiliwa kuingia eneo hilo kwa maelezo kinachojadiliwa ni siri.

“Wamenizuia nisiingie, wamesema nisubiri hadi watakapomaliza halafu nijaribu kuongea na baadhi ya washiriki wa kikao hicho kama watakuwa wameruhusiwa  kuzungumia hicho wanachokijadili…wanasema ni siri kubwa” alisema Kasembe

KUSINI ilibahatika kunasa sehemu ya mazungumzo ya Mkapa kwa viongozi hao ambapo yalionesha kutounga mkono hoja ya wananchi ya kupinga gesi kwenda Dar es Salaam.

Mkapa “Acheni kugombana na kusumbuana kwa kitu kisichojulikana, gesi mnayolumbana nayo si ya kutumika leo wala mwaka kesho na haijulikani kiasi ganiipo,mwaacha kujijenga kwenye korosho zao linalojulikana na linalotoa manufaa kwa wakazi wetu mnagombania gesi”

Aliongeza kuwa “Mimi sitaki kusikia wala kusimuliwa habari hiyo”

Aidha akizungumzia mgawanyiko ndani ya chama kuhusu gesi Mkapa aliwapa kazi wenyeviti wote wa wilaya na mkoa kutoa tofauti zilizopo pamoja na makundi huku akiwatakawampelekee majina ya wale  wote wanaoendelea kukivuruga chama.

Habari za awali zilidai kuwa Mbunge wa Mtwara Vijijini alimlalamikia Mkapa kuwa wabunge wenzake wamemsaliti kwa kuonesha kuwa ni yeye pekee ndiye aliyeruhusu gesi kwenda Dar es Salaam, hali iliyozaa makundi ndani ya chama.

Ghasia anadaiwa kumshitakia Mkapa Desemba, 19 alipofika jimboni kwake kukabidhi nyumba 30 za watumishi wa afya, hafla iliyofanyika kijiji cha Imekuwa Mtwara vijijini.

Wabunge kadhaa waliohojiwa na KUSINI walithibitisha kufanya kikao na rais huyo mstaafu lakini walikana kuzungumzia hoja zilizokuwa zikijadiliwa ndani ya kikao hicho kwa maelezo kuwa ni siri.

“Ni kweli nilikuwa Masasi kwenye kikao na Mkapa….siwezi kukuambia tulizungumza nini” alisema mmoja wa wabunge hao

Mwisho

Advertisements